Ushangialia wa goli wa mshambuliaji wa
Chelsea Samuel Eto'o umekuwa gumzo baada ya hapo jana kupachika bao
na kushangilia kama kikongwe huku akishika mti wa kwenye kona kama
mkongojo, katika mchezo ambao Chelesea ilishindia 4-0 Tottenham.
Eto'o ambaye amekuwa akilaumiwa kuwa ni
kikongwe, ambaye pia hata kocha wake Jose Mourinho alinukuliwa
akisema kwa mzaha kuwa Eto'o ni kama mchezaji mwenye umri wa miaka
35, alipachika bao hilo huku akiwa ametimiza umri wa miaka 33 siku ya
Jumatatu.
Hapa 'Kikongwe' Eto'o akipachika bao hilo murwa.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni