.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Siasa. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Siasa. Onyesha machapisho yote

Jumatano, 11 Aprili 2018

CCM MANISPAA YA IRINGA YATUMIA ZAIDI YA MILIONI TANO KUTATUA BAADHI YA CHANGAMOTO KATIKA HOSPITAL YA FRELIMO

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi manispaa ya Iringa (CCM) Said Rubeya akikambizi vifaa kwa ajili ya kutatua baadhi ya changamoto kwa kununua mashine mbili za umeme za kufulia nguo zenye thamani ya shilingi milioni tatu (3,000,000) na televisheni moja aina ya LG nchi 43 yenye thamani ya shilingi milioni mbili na laki mbili (2,200,000) ili kuboresha maisha ya wananchi wanaohudumiwa na hospital hiyo
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi manispaa ya Iringa (CCM) Said Rubeya akikambizi vifaa kwa ajili ya kutatua baadhi ya changamoto kwa kununua mashine mbili za umeme za kufulia nguo zenye thamani ya shilingi milioni tatu (3,000,000) na televisheni moja aina ya LG nchi 43 yenye thamani ya shilingi milioni mbili na laki mbili (2,200,000) ili kuboresha maisha ya wananchi wanaohudumiwa na hospital hiyo
Baadhi ya wananchi,makada wa chama cha mapinduzi mkoa wa Iringa na viongozi wa chama hicho waliokuwa wameudhulia makabidhiano ya vifaa kati ya uongozi wa hospital na viongozi wa chama hicho manispaa ya Iringa.

Na Fredy Mgunda,Iringa.

CHAMA cha mapinduzi manispaa ya Iringa kimetumia zaidi ya shilingi million tano kuanza kutatua baadhi ya changamoto zinazoikabili hospitali ya Frelimo iliyopo wilaya ya Iringa kwa kununua mashine mbili za kufulia na televisheni moja aina ya LG nchi 43.

Akizungumza wakati wa kukatibidhi vifaa hivyo mwenyekiti wa chama cha mapinduzi manispaa ya Iringa Said Rubeya alisema kuwa hospital hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi hivyo wameamua kuanza kuzitatua kwa awamu na kuangalia vipaumbele stahili.

“Tulikuja kwenye ziara hapa na viongozi wangu na tulikutana na viongozi wa hospatali hii wakatueleza changamoto nyingi sana ambazo ni ngumu kutekeleza kwa siku moja hivyo tulitoka na vipaumbele vyetu sisi kama chama ndio maana leo tumenza na hili na tutafuta na jingine” alisema Rubeya

Awali akisoma risala kwa mgeni rasmi mganga mfawidhi wa hospital hiyo, Dr Pilila Zambi alisema kuwa hospital hiyo inakabiliwa na changamoto zifuatazo jengo la vipimo na uchunguzi,wodi ya kulaza wagonjwa,wodi ya watoto,wodi ya kulaza wagonjwa wa magonjwa ya kuambukiza,jengo la utakasaji wa vifaa,jengo la kufulia nguo,nyumba za watumishi na ukosefu wa uzio.

Aidha Dr Zambi aliongeza kuwa hospital hiyo inaupungufu wa vifaa tiba ambavyo vimekuwa vikikamisha shughuli za kutoa huduma bora kwa wananchi,vifaa hivyo ni biochemistry machine,hematology machine Viral load analyser,Ultrasound machine na X-ray machine.

“Tukipata pia mashine kama mashine ya utakasaji, mashine ya kufulia na automatic genereta basi hapo tutakuwa tumefanikiwa kutatua changamoto za hospitali na tutatoa huduma bora kwa wananchi wanakuja kupata huduma katika hospital hii” alisema Zambi

Rubeya alisema kuwa kutokana na changamoto hizo ndio maana wameanza na kununua mashine mbili za umeme za kufulia nguo zenye thamani ya shilingi milioni tatu (3,000,000) na televisheni moja aina ya LG nchi 43 yenye thamani ya shilingi milioni mbili na laki mbili (2,200,000)

“Tuliona tuanze na vifaa hivi vidogo kwasababu inasikitisha kuona kuwa nguo chafu zenye vimelea vya magonjwa mbalimbali vinapitishwa katika ya mji hadi hospital ya Rufaa hivyo tukaamua kutatua kwa hii changamoto, pia wauguzi na madaktari mnatakiwa kujua nini kinaendelea nchi kwetu na nje ya nchi hiyo tukaamua kuwaletea TV hii kwa ajili ya mafunzo mbalimbali” alisema Rubeya

Akizungumza kwa niaba ya mstahiki meya diwani wa kata ya mivinjeni Frank Nyalusi amewataka viongozi wote kuleta maendeleo bila kujali itikadi za kisiasa na kuwashukulu viongozi wa chama cha mapinduzi kwa kuwafungulia njia ya maendeleo.

“Mimi binafsi niwapongezee chama cha mapinduzi kwa kazi kubwa mliyoifanya hapa kwa kutusaidia kutatua changamoto za hospital hii” alisema Nyalusi

Jumatatu, 9 Aprili 2018

KINANA AONGOZA VIONGOZI WA CCM MAOMBOLEZO YA WINNIE MADIKIZELA MANDELA.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Kanali Mstaafu Abdurahman Kinana akisaini kitabu cha maombolezo kwenyeOfisi za Ubalozi wa Afrika Kusini kufuatia kifo cha Mwanaharakati na mke wa zamani wa Rais wa kwanza Mwafrika wa Afrika Kusini(Hayati Nelson Mandela), Bi.Winnie Madikizela Mandela Jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Dkt Gaudensia Kabaka (MCC) akisaini kitabu cha maombolezo kwenyeOfisi za Ubalozi wa Afrika Kusini kufuatia kifo cha Mwanaharakati na mke wa zamani wa Rais wa kwanza Mwafrika wa Afrika Kusini(Hayati Nelson Mandela), Bi.Winnie Madikizela Mandela Jijini Dar es Salaam leo.
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga akisaini kitabu cha maombolezo kwenye Ofisi za Ubalozi wa Afrika Kusini kufuatia kifo cha Mwanaharakati na mke wa zamani wa Rais wa kwanza Mwafrika wa Afrika Kusini(Hayati Nelson Mandela), Bi.Winnie Madikizela Mandela Jijini Dar es Salaam leo.

Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Ndg.Shaka Hamdu Shaka akisaini kitabu cha maombolezo kwenye Ofisi za Ubalozi wa Afrika Kusini kufuatia kifo cha Mwanaharakati na mke wa zamani wa Rais wa kwanza Mwafrika wa Afrika Kusini(Hayati Nelson Mandela), Bi.Winnie Madikizela Mandela Jijini Dar es Salaam leo.

Jumatatu, 26 Machi 2018

KINANA AZINDUA SEMINA ELEKEZI KWA WAJUMBE WA BARAZA KUU LA UVCCM TAIFA LEO JIJINI DODOMA.

Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg.Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akizungumza kabla ya Kumkaribisha Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Ndg.Kheri Denis James (MCC) Kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Kufungua Semina Elekezi kwa Wajumbe wa Baraza kuu la Umoja wa Vijana Wa Chama cha Mapinduzi leo Mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg.Kheri Denis James(MCC) akizungumza wakati wa kutoa maelezo na kumkaribisha Mgeni Rasmi kufungua mafunzo Maalum kwa Wajumbe wa Baraza kuu la UVCCM Taifa.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akifungua semina elekezi kwa wajumbe wa Baraza kuu la Umoja wa Vijana wa CCM Taifa leo katika Ukumbi wa NEC katika Jengo la Ofisi ya Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma
Washiriki wakifuatilia semina elekezi kwa wajumbe wa Baraza kuu la Umoja wa Vijana,leo katikaUkumbi wa NEC Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.
Washiriki wakifuatilia semina elekezi kwa wajumbe wa Baraza kuu la Umoja wa Vijana,leo katikaUkumbi wa NEC Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.
Washiriki wakifuatilia semina elekezi kwa wajumbe wa Baraza kuu la Umoja wa Vijana,leo katikaUkumbi wa NEC Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.

Ijumaa, 23 Machi 2018

NAIBU KATIBU MKUU UWT EVA KIHWELE AMEVUNA WANACHAMA WAPYA ZAIDI 300 KATIKA TARAFA YA MAZOMBE MKOANI IRINGA

Naibu katibu mkuu bara wa umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi (UWT) taifa Eva Kihwele akiongea na wananchi pamoja na wanachama wa chama cha mapinduzi Tarafa ya mazombe wakati wa ziara ya viongozi wa UWT taifa akiwa sambamba na viongozi wa umoja huo mkoani IringaNaibu katibu mkuu bara wa umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi (UWT) taifa Eva Kihwele akiwapatia kadi wanachama wapya wa umoja wa chama cha mapinduzi Tarafa ya mazombe wakati wa ziara ya viongozi wa UWT taifa akiwa sambamba na viongozi wa umoja huo mkoani Iringa
Naibu katibu mkuu bara wa umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi (UWT) taifa Eva Kihwele pamoja na wanachama wa chama cha mapinduzi Tarafa ya mazombe wakati wa ziara ya viongozi wa UWT taifa akiwa sambamba na viongozi wa umoja huo mkoani Iringa wakiwasindikiza wanachama wapya kula kiapo cha kukitumikia chama hicho
Katibu wa umoja wa wanawake wa Ccm (UWT) wilaya ya Kilolo Judith Laizer akiwaonge na wananchi pamoja na wanachama wakati wa ziara ya viongozi wa UWT taifa.
Na Fredy Mgunda,Iringa.

NAIBU katibu mkuu bara wa umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi (UWT) taifa Eva Kihwele amevuna wanachama wapya zaidi ya mia tatu (300) katika tarafa ya Mazombe wilayani Kilolo mkoani Iringa ambo wamejiunga rasmi na umoja huo.

Wanachama hao wamepokelewa wakati wa ziara ya viongozi wa ngazi za juu wa UWT taifa mkoani Iringa, ambapo naibu katibu mkuu bara Eva Kihwele alipokuwa akiongea na wanachama pamoja na wananchi wa tarafa ya Mazombe ndipo waliposhawishika kujiunga na umoja huo kutokana na hamasa walioipata kutoka kwa katibu huyo.

Kihwele alisema kuwa chama cha mapinduzi ni chama ambacho kimejengwa kimisingi ya kulea jumuhia mbalimbali ambazo zipo ndani ya chama hicho ndio maana bado kinanguvu katika siasa za hapa nchini hata kimekuwa mfano kwa nchi nyingine.

“Jumuiya ya umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi Tanzania ni moja kati ya jumuiya ambayo ipo ndani ya chama hiki na inakazi zake kwa ajili ya kukijenga chama na kuleta maendeleo kwa wananchi waliokipa dhamana ya kuongoza nchi hii” alisemaKihwele

Aidha Kihwele aliwataka wanawake kujifunza kujifunza kujitegemea ili waweze kuja kuwaajiri wanaume ambao kwa sasa ndio wamekuwa wakitoa ajira nyingi kwa wanawake hapa nchini.

“Wanawake wenzangu sasa imefika mwisho wa kuwa tegemezi kwa wanaume inatakiwa sasa tusimame sisi kama sisi na tuanze kuwaajiri na kulisha wanaume zenu majumbani kwetu maana tunauwezo wa kufanya kila kazi hizo inatakiwa tujitume” alisemaKihwele

Kihwele alisema kuwa wanawake mkiwa mnataka kufanya biashara zenye malengo msiogope kwenda kukopa maana siku hizi kuna mikopo ya bei rahisi na riba yake sio kubwa ambayo itakuwezesha kufanya biashara yako kwa maendeleo yako.
“Siku hizi kuna mabenk mengi yanawakopesha wanawake na wanawaamini sana wanawake kwenye kufanya biasha hivyo nendeni mkakope msiogope maana hizi benk zipo kwa ajiri ya kusaidia kuinua maisha ya mtanzania” alisema Kihwele

Kihwele alimalizia kwa kuwataka wanawake wa kata ya Mkwawa mkoani Iringa kuzitumia pesa kwa nidhamu ya hali ya juu ili ziweze kuleta matunda ya kuleta maendeleo ambayo yanahitajika kwa maisha yao.

“Jamani kila pesa ukiitumia kwa nidhamu basi utaona faida yake na itakuletea maendeleo yako na taifa kwa ujumla maana unakuwa umetumia vizuri pesa kwa maendeleo” alisema Kihwele

Kwa upande wake mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rose Tweve alisema kuwa atawapatia elimu ya ujasiliamali ili wakipata mitaji waweze kuitumia vizuri kwa ajili ya manufaa ya maendeleo.

“Jamani mimi nimekuwa nikitoa elimu ya ujasiliamali mara kwa mara kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kufanya biashara zenu kwa faida na kutoa elimu ya matumizi ya fedha hivyo nawaomba nikiitisha tena kutoa elimu mkaribia kwa wingi maana huwa inakuwa bure” alisema Twelve

Naye Katibu wa umoja wa wanawake wa Ccm (UWT) wilaya ya Kilolo Judith Laizer amewataka wanawake kote nchini kujikwamua kiuchumi kwa kufanya shughuli ndogo ndogo za ujasiriliamali ili kuachana na utegemezi.

Laizer alisema kuwa baadhi ya wanawake hasa wa vijiji wamekuwa wakipata msongo wa mawazo kutokana na kutokuwa na kipato licha ya kushiriki shuhuli za uzalishaji mali ngazi ya familia lakini wengi wao wamekuwa hawashirikishwi katika matumizi ya kipato walichokitolea jasho.

Laizer alisema kuwa kuna mifuko maalumu ya kuwaisidia wanawake hasa wa hali ya chini kwa kuwapatia mitaji kupitia vikundi ili kuanzisha biashara ndogo ndogo na kuachana na utegemezi hivyo msaada walioupata utawafanya wapige hatua kubwa zaidi.

Jumatano, 21 Machi 2018

MNEC MWAKA RAMADHAN AMEVUNA WANACHAMA WAPYA (80) KATA YA MKWAWA MANISPAA YA IRINGA

 Mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi (CCM) Taifa na mjumbe wa kamati utekelezaji wa UWT taifa Mwaka Ramadhan akiongea na wanawake waliokuwa wamejitokeza kumsikiliza kwenye ziara ya UWT taifa mkoani Iringa katika Kata ya Mkwawa
Baadhi ya wanachama waliojiunga na umoja wa wanawake UWT katika kata ya Mkwawa wakatika wa ziara ya viongozi wa kitaifa mkoani Iringa
Baadhi ya wanachama wa chama cha mapinduzi wakiwa katika kitendo cha kula kiapo pamoja na wanachama waliojiunga na umoja wa wanawake UWT kata ya Mkwawa
Mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi (CCM) Taifa na mjumbe wa kamati utekelezaji wa UWT taifa Mwaka Ramadhan akiwa na mbunge wa viti maalum Ritta Kabati pamoja na mwenyekiti wa UWT manispaa ya Iringa Ashura Jongo Pamoja katibu wa UWT manispaa ya Iringa

Na Fredy Mgunda,Iringa

MJUMBE wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi (CCM) Taifa na mjumbe wa kamati utekelezaji wa UWT taifa Mwaka Ramadhan amevuna wanachama wapya zaidi ya themanini (80) katika kata ya Mkwawa Manispaa ya Iringa ambo wamejiunga rasmi na umoja huo.

Wanachama hao wamepokelewa wakati wa ziara ya viongozi wa ngazi za juu wa UWT taifa mkoani Iringa, ambapo MNEC Ramadhan alipokuwa akiongea na wanachama pamoja na wananchi wa kata ya Mkwawa ndipo waliposhawishika kujiunga na umoja huo kutokana na hamasa walioipata kutoka kwa MNEC huyo.

Ramadhan alisema kuwa chama cha mapinduzi ni chama ambacho kimejengwa kimisingi ya kulea jumuhia mbalimbali ambazo zipo ndani ya chama hicho ndio maana bado kinanguvu katika siasa za hapa nchini hata kimekuwa mfano kwa nchi nyingine.

“Jumuiya ya umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi Tanzania ni moja kati ya jumuiya ambayo ipo ndani ya chama hiki na inakazi zake kwa ajili ya kukijenga chama na kuleta maendeleo kwa wananchi waliokipa dhamana ya kuongoza nchi hii” alisema Ramadhan

Aidha Ramadhan aliwataka wanawake kujifunza kujifunza kujitegemea ili waweze kuja kuwaajiri wanaume ambao kwa sasa ndio wamekuwa wakitoa ajira nyingi kwa wanawake hapa nchini.

“Wanawake wenzangu sasa imefika mwisho wa kuwa tegemezi kwa wanaume inatakiwa sasa tusimame sisi kama sisi na tuanze kuwaajiri na kulisha wanaume zenu majumbani kwetu maana tunauwezo wa kufanya kila kazi hizo inatakiwa tujitume” alisemaRamadhan
Ramadhan alisema kuwa wanawake mkiwa mnataka kufanya biashara zenye malengo msiogope kwenda kukopa maana siku hizi kuna mikopo ya bei rahisi na riba yake sio kubwa ambayo itakuwezesha kufanya biashara yako kwa maendeleo yako.

“Siku hizi kuna mabenk mengi yanawakopesha wanawake na wanawaamini sana wanawake kwenye kufanya biasha hivyo nendeni mkakope msiogope maana hizi benk zipo kwa ajiri ya kusaidia kuinua maisha ya mtanzania” alisema Ramadhan

Ramadhan alimalizia kwa kuwataka wanawake wa kata ya Mkwawa mkoani Iringa kuzitumia pesa kwa nidhamu ya hali ya juu ili ziweze kuleta matunda ya kuleta maendeleo ambayo yanahitajika kwa maisha yao.

“Jamani kila pesa ukiitumia kwa nidhamu basi utaona faida yake na itakuletea maendeleo yako na taifa kwa ujumla maana unakuwa umetumia vizuri pesa kwa maendeleo” alisema Ramadhan
Kwa upande wake mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati alisema kuwa atawapatia elimu ya ujasiliamali ili wakipata mitaji waweze kuitumia vizuri kwa ajili ya manufaa ya maendeleo.

“Jamani mimi nimekuwa nikitoa elimu ya ujasiliamali mara kwa mara kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kufanya biashara zenu kwa faida na kutoa elimu ya matumizi ya fedha hivyo nawaomba nikiitisha tena kutoa elimu mkaribia kwa wingi maana huwa inakuwa bure” alisema Kabati

Jumatatu, 19 Machi 2018

WAZAZI WALEENI WATOTO WENU KATIKA MAADILI NA TAMADUNI ZA KITANZANIA

Naibu Katibu Mkuu Wazazi ccm Tanzania bara Godfrey Mheluka akiwa anawahutumia wananchi waliouthuria katika kongamano la kujadili maadili mema na uzalendo ni ustawi wa Arusha yetu na Taifa letu kwa ujumla ,kongamano lililoandaliwa na Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM)mkoa wa Arusha ,kongamano ambalo lilishirikisha wananchi ,viongozi wa dini ,vyombo vya usalama pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na wa sekta binafsi iliyofanyikia katika ukumbi wa Triple A uliopo ndani ya jiji la Arusha
Kamanda wa vijana UVCCM mkoa wa Arusha Philemon Molel maarufu kama Monabani akiongea na wananchi waliouthuria katika kongamano la kujadili maadili mema na uzalendo ni ustawi wa Arusha yetu na Taifa letu kwa ujumla ,kongamano lililoandaliwa na Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM)mkoa wa Arusha ,kongamano ambalo lilishirikisha wananchi ,viongozi wa dini ,vyombo vya usalama pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na wa sekta binafsi iliyofanyikia katika ukumbi wa Triple A uliopo ndani ya jiji la Arusha
                                                               
                                                             Habari picha na Woinde Shizza,Arusha

Wazazi wametakiwa kutimiza wajibu wao wa kuwalea watoto kwakufuata
maadili ya Mtanzania na kuacha kuiga tamaduni za kigeni ,kwani baadhi ya tamaduni za kigeni wanazo ziiga zinachangia kusababisha mporomoko wa maadili katika jamii zetu .

Hayo yamebainishwa na Naibu Katibu Mkuu Wazazi ccm Tanzania bara
Godfrey Mheluka wakati akifunga kongomano la kujadili maadili mema
na uzalendo ni ustawi wa Arusha yetu na Taifa letu kwa ujumla ,kongamano lililoandaliwa na Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Arusha ,kongamano ambalo lilishirikisha wananchi ,viongozi wa dini ,vyombo vya usalama pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na wa sekta binafsi iliyofanyikia katika ukumbi wa Triple A uliopo ndani ya jiji la Arusha

Alisema kuwa wazazi wengi wa wamekuwa wanalea watoto kwa kufuata
tamaduni za wenzetu wan chi za nje wakidai kuwa ndio malezi bora kwa
watoto na yakisasa kitu ambacho sio kizuri kwani baadhi ya tamaduni za
wenzetu ukiangalia za kutoka nchi za kimagharibi zinaporomosho maadili kwa watoto wetu.

“ukithamini tamaduni za kimagharibi na ukaacha za kwetu na ukamuacha
mtoto nae akathamini tamaduni hizohizo ujue umempoteza mtoto na
umemuaribu kabisa unakuta mzazi anaona mtoto anavaa mlegezo au kimini
badala ya kumkataza anamuacha anaona kuwa wake ndio mjanja huo sio
ujanja ni ujinga ni kumuaribu mtoto unatakiwa umwambie mtoto hivi sio vyema ivi nikiwauliza wazazi ivi nyie mngelelewa hivyo au mngelelewa vibaya je leo mngekuwepo apo mlipo ni wajibu wetu kuwalea watoto wetu kwa kufuata utamaduni wetu mzuri wenye maadili ili kuweza kuandaa viongozi wazuri wa baada na wazazi wazuri wa baadae “alisema Mhekuka

Kwa upande wake mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi ccm mkoa wa Arusha
Dr,John Palanjo alisema ni wazazi anatakiwa kutimiza waji wake kwa mtoto wake huku pia mtoto akitakiwa kutimiza wajibu wake kwa mzazi ,aliongeza kuwa pia niwajibu wa kila mzazi kumfatilia mtotowake na kujua maendeleo yake mwenyewe na sio kumuachia mwalimu amfatilie au dada wa kazi amfatilie huku akibainisha kuwa mzazi yeyote asitafute mchawi wa mtoto wake kwani ,asilimia kubwa ya wazazi wao wenyewe ndio
wachawi wawatoto wao.

Aidha aliwaasa wazazi kutenga mda wa kukaa na watoto wao na kuongea na
kuwaelezea kipi kibaya na kipi kizuri ili kuwawezesha watoto wetu kukuwa kwa kuendana na yale yanayopendeza kwa jamii inayowazunguka

“mimi na imaini iwapo mzazi akijua wajibu wake atakubali hata kidogo mtoto wake aharibike ,hivyo ni vizuri mzazi utambue wajibu wako umrudie mungu usali maana ukiwa na hofu ya mungu lazima utamlea mtoto kwa kufuata kanuni za kimungu”alisema katibu wa wawazazi wilaya ya Arusha Christoper Pallangyo

Kwa upande wake mwenyekiti wa wazazi wilaya ya Arusha Ally Meku aliwataka baadhi ya wazazi kupunguza migogoro ndani ya familia ili watoto nao wasiige tabia mbaya kwani wanapoaanza migogo katika familia wanashindwa kuwale watoto wao na badala yake watoto hao wanaanza kutangatanga hovyo na kuanza kuiga tabia mbaya.

                                           Baadhi ya viongozi wakiwa wanaimba na kucheza

Jumanne, 13 Machi 2018

MNEC SALIMU ASAS ATOA SHILINGI MILIONI KUMI NA TATU (13,000,000) KWA AJILI YA MAENDELEO YA UWT IRINGA MJINI

Mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas akiongea na wajumbe wa baraza la UWT manispaa ya Iringa lilofanyika katika ukumbi wa CCM sabasaba na kutoa jumla ya shilingi milioni
kumi na tatu(13,000,000) kwa UWT Iringa Mjini
Mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas akipokea zawadi kutoka kwa viongozi wa UWT manispaa ya Iringa
Mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas akibadilisha mawazo na mwenyekiti wa UWT manispaa ya Iringa Ashura Jongo pamoja na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati.

Na Fredy Mgunda,Iringa.

MJUMBE wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas ameendelea kuineemesha jumiya ya umoja wa wanawake mkoa wa Iringa (UWT) kwa kutoa kiasi cha shilingi milioni nne (4,000,000) kwa jumuiya hiyo wilaya ya Iringa Mjini kwa ajili ya kuendeleza miradi ya umoja huo na kuondokana kuwa tegemezi.

Pesa hizo zimetolewa wakati wa baraza la umoja wa wanawake wilaya ya Iringa Mjini mkoani (UWT) lilofanyika katika ukumbi wa chama cha mapinduzi ulipo Iringa Mjini na kuhudhuriwa na wageni wengi wakiwepo wabunge wa viti maalum ambao ni Ritta Kabati na Rose Tweve

Akizungumza katika baraza hilo MNEC Asas alisema kuwa amependezwa na mikakati ambayo imefanya na umoja huo wa wilaya ya Iringa Mjini kwa kuwa wanafanya kazi na viongozi pamoja na wananchi wa chini hivyo inakuwa rahisi kuendelea kukijenga chama hicho.

Nimeona kwenye hotuba yenu mmesema kuwa “mtahakikisha kuwa wanawake wanajiunga kwenye vikundi vya uzalishaji kama vile vikoba ,saccos na vikundi vingine ili waweze kupata mafunzo stahiki ya ujasiliamali kwa lengo la kupambana na hali ya kiuchumi na kuongeza kipato,”hakika kwa kufanya hivi mtawaokoa wanawake wengi sana kiuchumi. Alisema Asas

Asas alisema kuwa nimesikia mnataka kuanzisha duka kwa ajili ya kuongeza ajira na kuongeza uchumi wa umoja huu,hilo ni jambo bora hivyo kwa kuona mikakati hiyo nawachangia kiasi cha shilingi milioni nne (4,000,000) ili wafikie malengo ya kujiendesha na kuacha kuwa tegemezi.

Aidha Asas alimpongeza mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Rose Twelve kwa jitihada alizozifanya za kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kutoa mitaji kwenye kata kumi na saba kwa kutoa kiasi cha shilingi laki sita kwa kila kata,hivyo kwa kuliona hilo MNEC alisema kuwa atachangia kiasi cha shilingi laki tano kwa kila kata hivyo kwa kata zote 18 za wilaya ya Iringa Mjini atachangia kiasi cha shilingi milioni tisa (9,000,000).

Kwa hili sipepesi macho nampongeza sana mbunge Rose Tweve kwa kazi kubwa anayoifanya kuhakikisha wanawake wanapata mafanikio kwa kuwawezesha kama alivyofanya kwa kufanya hivyo amefanikiwa kuwafikia wanawake walio na kipatao cha chini kabisa na nitaendelea kukusaidia mbunge kwa kazi unazozifanya kwa ajili ya maendeleo” alisema Asas
Kwa upande wake katibu wa UWT wilaya ya Iringa Mjini Frola Kapalia alimshikuru MNEC Salim Asas kwa kutoa msaada mkubwa kama huo ambao hata wao hawakutegemea kutokea kitu kama hicho,ambapo ukipiga mahesabu utagundua kuwa ametoa jumla ya shilingi milioni kumi na tatu(13,000,000) kwa UWT Iringa Mjini

“Ametoa shilingi mioni nne kwa UWT na ametoa milioni tisa (9,000,000) kwa ajili ya kuongezea nguvu kwenye mfuko wa mbunge Rose Tweve hivyo lazima tujivunie kuwa na MNEC wa namna hii” alisema Kapalia

Jumapili, 11 Machi 2018

MNEC SALIM ASAS BADO ANAUMIZWA NA USHINDI WA MBUNGE MSIGWA WA MWAKA 2015

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) MNEC Salim Asas akiwahutubia wajumbe wa baraza kuu la umoja wa wanawake manispaa ya Iringa na kusema kuwa bado anaumizwa na matokeo ya ubunge wa jimbo la Iringa mjini baada ya wapinzani kushinda kwa kishindo mwaka 2015 kwa ni kitendo ambacho hakukitegemea.
Mwenyekiti wa umoja wa wanawake UWT manispaa ya Iringa Ashura jongo akimtoa hofu MNEC Salim Asas juu ya kukomba jimbo baada ya kulipoteza kwa kusalitia mwaka 2015
Baadhi ya wageni waliokuwa wamealikwa kwenye baraza hilo kwa ajili ya kujifunza na kutoa mapendekezo pale wanapopata nafasi
Baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi mkoani Iringa walipokuwa wakimsikiliza kwa umakini mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) MNEC Salim Asas alipokuwa anatoa ya moyo kuhusu kushindwa katika uchaguzi wa mwaka 2015

Na Fredy Mgunda,Iringa.

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) MNEC Salim Asas bado anaumizwa na matokeo ya ubunge wa jimbo la Iringa mjini baada ya wapinzani kushinda kwa kishindo mwaka 2015 kwa ni kitendo ambacho hakukitegemea.

Akizungumza wakati wa baraza la UWT manispaa ya Iringa Asas alisema kuwa usaliti ulifanywa katika uchaguzi wa mwaka 2015 umekuwa ukimuumiza hadi sasa na kitendo anafikiri kitadumu moyoni mwake hata kwa miaka kumi kwakuwa bado anakumbuka mara kwa mara.

“Naombeni niongee ukweli kitendo kilichofanywa na wanaccm wa manispaa ya Iringa katika uchaguzi wa mwaka 2015 kilikuwa kitendo ambacho ni usaliti mkubwa ambao unaumiza sana kichwa changu” alisema Asas

Asas alisema kuwa uchaguzi huo kulikuwa na wanaccm wengi ambao mchana walikuwa ccm na usikuwa walikuwa kwa wapinzani hivyo lazima tuondoe usaliti kwenye chama bila hivyo tutaendelea kushindwa kila siku.

“Unakuta rasilimali zilizokuwa zinatolewa na chama cha mapinduzi zote zinatumika kwa wapinzani kuhakikisha wanaiangusha ccm,sasa hicho kitu ndio ambacho kinaniumiza sana kichwa hadi hii leo” alisema Asas

Asas aliutaka umoja wa wanawake (UWT) manispaa ya Iringa kufanya kazi kwa umoja unatakiwa na kuhakikisha kuwa ccm inakuwa ila na isiyo na makundi ili kufika mwaka wa uchaguzi wanashinda kwa kishindo kwa kutumia umoja wao.

“Nawaombe muutunze umoja huu ambao sasa mnao hadi kipindi cha uchaguzi wowote ule ambao upo mbele yetu na kuhakikisha kuwa tunashinda kila chaguzi kwa kishindo kwa kuwa nyie akina mama ndio huwa mnakula ambazo haziamishiki” alisema Asas

Kwa upande wake mwenyekiti wa UWT manispaa ya Iringa Ashura jongo alimuhakikishia MNEC Salim Asas kuwa kosa lilofanyika mwaka 2015 halitajirudia tena katika chaguzi yoyote ambayo itakuwa inafanyika katika manispaa ya Iringa.

“Ndugu MNEC kwa kweli tumejifunza na tunajutia kitu kilichofanyika mwaka 2015 hivyo tunakuhadi kuwa kwenye umoja wetu wa wanawake Manispaa ya Iringa hakitaa tokea kama kilivyotokea,na tutashinda chaguzi zetu kwa kuwa kila mtu anaumia na kilichotokea mwaka 2015” alisema Jongoo

Jongoo alimshukuru MNEC kwa kurudisha umoja kwa wanaccm mkoa wa Iringa kwa kuwa anafanya kazi kubwa kuhakikisha kila kitu kinakuwa kama kinavyokusudiwa na kuhakikisha umoja ambao umetengenezwa na viongozi wapya unadumu hadi watakapomaliza uchaguzi.

“Mheshimiwa MNEC umoja ambao tunao hivi sasa tunatakiwa kuulinda na kuudumisha hadi kipindi cha chaguzi zote na kuhakikisha kuwa ccm inashinda kwa kushinda na kuendelea kuwa ngoja ya chama hicho kama ilivyokuwa hapo awali” alisema Jongoo

Jumatatu, 5 Machi 2018

MNEC SALIM ASAS ATOA MILIONI 24 KWA AJILI YA MAENDELEO YA UWT WILAYA YA MUFINDI

Mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas ameendelea kuineemesha jumiya ya umoja wa wanawake mkoa wa Iringa (UWT) kwa kutoa kiasi cha shilingi milioni sita (6,000,000) kwa jumuiya hiyo wilaya ya Mufindi kwa kutoa kiasi cha shilingi milioni sita kwa ajili ya kuendeleza miradi ya umoja huo na kuondokana kuwa tegemezi. Mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas akikabidhiwa shati na umoja wa wanawake (UWT) wilaya ya Mufindi baada ya kukabidhiwa kofia ambayo ameifaa hapo
Mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas akifurahia jambo na viongozi wa chama hicho pamoja na wabunge wa viti maalum mkoa wa Iringa.

Na Fredy Mgunda,Iringa.

MJUMBE wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas ameendelea kuineemesha jumiya ya umoja wa wanawake mkoa wa Iringa (UWT) kwa kutoa kiasi cha shilingi milioni sita (6,000,000) kwa jumuiya hiyo wilaya ya Mufindi kwa kutoa kiasi cha shilingi milioni sita kwa ajili ya kuendeleza miradi ya umoja huo na kuondokana kuwa tegemezi.

Pesa hizo zimetolewa wakati wa baraza la umoja wa wanawake wilaya ya Mufindi mkoani (UWT) lilofanyika katika ukumbi wa chama cha mapinduzi ulipo mjini Mafinga na kuhudhuriwa na wageni wengi wakiwepo wabunge wa viti maalum ambao ni Ritta Kabati,Rose Tweve na mama Mwamwindi.

Akizungumza katika baraza hilo MNEC Asas alisema kuwa amependezwa na mikakati ambayo imefanya na umoja huo wa wilaya ya mufindi kwa kuwa wanafanya kazi na viongozi pamoja na wananchi wa chini hivyo inakuwa rahisi kuendelea kukijenga chama hicho.

Nimeona kwenye hotuba yenu mmesema kuwa “mtahakikisha kuwa wanawake wanajiunga kwenye vikundi vya uzalishaji kama vile vikoba ,saccos na vikundi vingine ili waweze kupata mafunzo stahiki ya ujasiliamali kwa lengo la kupambana na hali ya kiuchumi na kuongeza kipato,”hakika kwa kufanya hivi mtawaokoa wanawake wengi sana kiuchumi. Alisema Asas

Asas alisema kuwa nimesikia mnataka kujenga kipanda kwa ajili ya kuongeza ajira na kuongeza uchumi wa umoja huu,hilo ni jambo bora hivyo kwa kuona mikakati hiyo nawachangia kiasi cha shilingi milioni sita ili mfikie malengo yenu.

“Sijaona changamoto ila nimeona matarajio ambayo ni kuanzisha mradi wa kuuza sare za chama,kumalizia ujenzi wa vibanda vya umoja wenu,kutafuta eneo la ekar 5 kwa ajili ya kilimo cha viazi na kupanda miche ya miparachichi na kutafuta kiwanja kikubwa kwa ajili ya uwekezaji na ndio sababu iliyonifanya niwachangie kiasi hicho cha pesa” alisema Asas

Aidha Asas alimpongeza mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Rose Twelve kwa jitihada alizozifanya za kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kutoa mitaji kwenye kata kumi na saba kwa kutoa kiasi cha silingi laki sita kwa kila kata,hivyo kwa kuliona hilo MNEC alisema kuwa atachangia kiasi cha shilingi laki tano kwa kila kata kwa kata zote 36 za wilaya ya Mufindi.

Kwa hili sipepesi macho nampongeza sana mbunge Rose Tweve kwa kazi kubwa anayoifanya kuhakikisha wanawake wanapata mafanikio kwa kuwawezesha kama alivyofanya kwa kufanya hivyo amefanikiwa kuwafikia wanawake walio na kipatao cha chini kabisa na nitaendelea kukusaidia mbunge kwa kazi unazozifanya kwa ajili ya maendeleo” alisema Asas
Kwa upande wake katibu wa UWT wilaya ya Mufindi Mwanaidi Kaleghela alimshikuru MNEC Salim Asas kwa kutoa msaada mkubwa kama huo ambao hata wao hawakutegemea kutokea kitu kama hicho,ukipiga mahesabu utagundua kuwa ametoa milioni ishirini na nne kwa UWT mufindi.
“Ametoa shilingi mioni sita kwa UWT na ametoa milioni kumi na nane kwa ajili ya kuongezea nguvu kwenye mfuko wa mbunge Rose Tweve hivyo lazima tujivunie kuwa na MNEC wa namna hii” alisema Kaleghela

MNEC SALIM ASAS AMPONGEZA MBUNGE ROSE TWEVE KWA KUINUA UCHUMI WA WANAWAKE WA WILAYA YA MUFINDI.



Mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas amempongeza mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Rose Tweve kwa kuinua uchumi wa wananchi kwa kutoa kiasi cha shilingi laki sita (600,000) kwa kata kumi na saba za wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringakupitia chama cha mapinduzi Rose Tweve akiongea mbele ya baraza kwa kuonyesha furaha yake mbele ya mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas baada ya kuambiwa kuwa ataongezewa shilingi milioni kumi na nane kwa ajili ya maendeleo ya akina wanawake wa wilaya ya Mufindi
Viongozi mbalimbali na wabunge wa viti maalum walihudhuria baraza hilo.

Na Fredy Mgunda,Iringa.

MJUMBE wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas amempongeza mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Rose Tweve kwa kuinua uchumi wa wananchi kwa kutoa kiasi cha shilingi laki sita (600,000) kwa kata kumi na saba za wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.

Akingumza wakati wa baraza la UWT wilaya ya Mufindi Salim Asas alisema kuwa amefurahishwa na mkakati mbunge Rose Tweve kwa kufanikiwa kuwafikia wananchi wa kipato cha chini kabisa ambao ndio wanastahili kuinuliwa kiuchumi kuliko wananchi ambao tayari wanauchumi mkubwa.

“Kwa kweli niwe muwazi kuwa nimefurahishwa na hiki kitu ambacho huyu mbunge anakifanya kwa kuwawezesha wananchi ambao ndio serikali ya awamu ya tano inataka kuwafikia na kuwainua kiuchumi” alisema Asas

Asas aliwata wabunge wengine kuiga mfano wa mbunge Tweve kwa kazi anayoifanya ya kuwawezesha akina mama na wananchi wengi kwa kuwa hiyo ndio inakuwa faida kwa taifa.
“Naombeni wabunge wangu wote tufanye kazi kama anayoifanya mbunge Rose Tweve kwa kuwafikia wananchi wa chini ambao mara nyingi imekuwa vigumu kuwafikia kutokana na sababu mbalimbali” alisema Asas

Aidha Asas alisema kutokana kazi kubwaanayoifanya mbunge Rose Tweve atachangia kiasi cha shilingi laki tano (500,000) kwa kila kata kwa kata zote 36 za wilaya ya Mufindi ambapo atatoa kiasi cha shilingi milioni kumi na nane (18,000,000) kwa ajili ya kuchangia vikundi hivyo.

Kwa hili sipepesi macho nampongeza sana mbunge Rose Tweve kwa kazi kubwa anayoifanya kuhakikisha wanawake wanapata mafanikio kwa kuwawezesha kama alivyofanya kwa kufanya hivyo amefanikiwa kuwafikia wanawake walio na kipatao cha chini kabisa na nitaendelea kukusaidia mbunge kwa kazi unazozifanya kwa ajili ya maendeleo” alisema Asas

Kwa upande wake katibu wa UWT wilaya ya Mufindi Mwanaidi Kaleghela alimshikuru MNEC Salim Asas kwa kutoa msaada mkubwa kama huo ambao hata wao hawakutegemea kutokea kitu kama hicho,ukipiga mahesabu utagundua kuwa ametoa milioni ishirini na nne kwa UWT mufindi.

Kaleghela alisema hadi kufika sasa mtaji umekuwa hadi kufikia shilingi milioni hamsini na mbili laki tano (52,500,000) na fedha hizo zinasimamiwa na umoja wa wanawake wilaya ya Mufindi (UWT)

Bila mchango wa mbunge Rose Tweve tusingeweza kuwafikia wananchi kwa kiasi hiki hivyo nachukua nafasi hii pia kumpongeza mbunge wetu kwa kazi anazozifanya kwa maendeleo ya wananchi.

Kwa upande wake mbunge Rose Tweve alikuwa ni mtu mwenye furaha baada ya kupokea hongera na kuchangiwa kiasi cha shilingi milioni kumi na nane (18,000,000) kutoka kwa MNEC.

“Mnaniona nabubujika machozi kutokana na furaha niliyonayo kutoka na mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas kutambua mchango wangu” alisema Tweve

Jumatano, 28 Februari 2018

CCM MANISPAA YA IRINGA YATEKELEZA AHADI YA MBUNGE MSIGWA KATIKA SOKO KUU LA MANISPAA YA IRINGA

Mwenyekiti wa chama cha mapindizi (CCM) manispaa ya Iringa Said Rubeya akimkabidhi TV na king'amuzi mwenyekiti wa masoko ya manispaa ya iringa Starmi Mathew akiwa sambamba na viongozi na wanachama wa chama hicho
Mwenyekiti wa chama cha mapindizi (CCM) manispaa ya Iringa Said Rubeya akimkabidhi king'amuzi mwenyekiti wa masoko ya manispaa ya iringa Starmi Mathew akiwa sambamba na viongozi na wanachama wa chama hicho
Mbunge wa viti maalumu ritta Kabati akiwa na diwani wa kata ya Mshindo Ngwada pamoja na matha walipokuwa wakikabidhi TV na king'amuzi cha Azam kwa viongozi wa soko kuu la manispaa ya Iringa
Wananchama wa chama cha mapinduzi pamoja na baadhi ya wafanyabiashara walipohudhuria hafla ya kukabidhiwa kwa TV na king'amuzi cha Azam TV kwa viongozi wa soko kuu manispaa ya Iringa.

Na Fredy Mgunda,Iringa.

CHAMA cha mapindizi (CCM) manispaa ya Iringa kimetekeleza ahadi ilikuwa imeahidiwa na chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) wakati wa kampeni za mwaka 2015 ya kuwatafutia TV wafanyabiashara wa soko kuu la manispaa ya Iringa chini ya mgombea wake wa ubunge mchungaji Petter Msigwa ambaye kwa sasa ndio mbunge wa jimbo la Iringa mjini

Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa CCM manispaa ya Iringa Said Rubeya alipokuwa anakabidhi TV nchi 58 na king’amuzi kwa kiongozi wa masoko hapa manispaa.

Rubeya alisema kuwa wametoa TV hiyo kwa lengo la kuhakikisha kuwa wananchi na wafanyabiashara wa soko hilo wanapata habari kwa wakati.

“Mimi nimekuja jana hapa mkaniambia kero hii nikaichuklua na chama change kimeifanyia kazi haraka iwezekanavyo na saizi tumekuja kukabidhi” alisema Rubeya

Rubeya alisema kuwa chama cha mapinduzi kinaamini kwenye utendaji na sio kulalamika na kuandamana hivyo kuna tumia vizuri falsafa ya Rais Dr John Pombe Magufuli ya hapa kazi tu ndio maana tupo hapa kufanya kazi kwa vitendo kwa wananchi.

“Chama cha mapinduzi manispaa ya Iringa kinafanya kazi kwa vitendo pale tunaposikia kero za wananchi tunatafuta njia za kutatua changamoto hizo ndio maana leo tunaleta hii TV na king’amuzi ili wafanyabiasha mpate habari mkiwa hapa kazini” alisema Rubeya

Rubeya alisema kuwa alipokea malalamiko kutoka kwa wafanyabiasha ya kutekelezwa kwa ahadi ambazo zilizotelewa na mbunge wakati kampeni na imepita miaka mingi haijatekelezwa hivyo wakaamua kuichua na kuitatua ili kuwapa haki wananchi na wafanyabishara wa soko hilo.

“CCM tukitoa ahadi tunatekeleza kwa wakati lakini wenzetu wamekuwa wanapiga propaganda tu za maneno hivyo wananchi mnatakiwa kuchagua viongozi ambao wanaweza kutekeleza ahadi zao kwa maendeleo ya wananchi wanaowangoza” alisema Rubeya

Kwa upande wake mbunge wa viti maalumu ritta Kabati alisema kuwa kitendo cha leo walichokifanya chama cha mapinduzi manispaa ya Iringa kinaonesha kuwa chama hicho ni chama cha wananchi wote ndio maana leo wametoa TV na king’amuzi kwa ajili ya kupata habari kwa wananchi wanaopata huduma katika soko hilo.

“Kupata habari ni haki ya kila mwananchi wa mtanzania anapata habari kwa wakati hivyo kutoa TV hii kutasaidia kuongeza wigo kwa wananchi kupata habari kwa wakati” alisema Kabati

Kabati aliwataka viongozi wa soko hili kuandaa mkutano wa kusikiza kero ili kuzitafutia ufumbuzi kwa lengo la kuendelea kukuza uchumi na kuleta maendeleo kwa haraka zaidi na kuendana na kasi ya Rais wa awamu ya tano Dr Johh Pombe Magufuli.

“Mwenyekiti naomba mniandalie mkutano nije kuwasikiliza kero zenu kwa kuwa ni haki yenu na msipofanya hivyo mtakuwa mnajinyima haki yenu ya msingi ya kutatuliwa kero zenu” alisema Kabati

Naye mwenyekiti wa masoko ya manispaa ya iringa Starmi Mathew aliwashukuru chama cha mapinduzi kwa msaada walioutoa kwa kuwa wamerahisisha wafanyabiashara kupata habari wakiwa kazini.

Mathew alikiomba chama hicho kuongezea nguvu kwenye masoko mwengine ya manipsaa ya Iringa kupata hata TV ndogo hata kama sio kuwa kama ambayo imetolewa leo katika soko kuu la manispaa ya Iringa

“Naomba nimbe kama hapo mbe mtapa nguvu nyingine basi tunaomba mtukumbuke tena maana kuna soko hilo hapo chini nalo linahitaji kuwa na Tv nao wewe kupata habari kama haki yao ya msingi kujia nini kinaendelea duniani” alisema Mathew

Aidha Mathew akawamba viongozi wa chama cha mapinduzi kuwasidia kuiomba SUMATRA kutengeneza njia ya daladala ipite katika soko hilo ili kuongeza mzunguko wa kibiashara kama ilivyo mikoa mingi hapa nchini.

Ijumaa, 9 Februari 2018

MSTAHIKI MEYA SELEBOSI AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI LEO JIJINI TANGA

Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga(CCM) Alhaji Mustapha Mhina Selebosi akizungumza wakati akifungua kikao cha Baraza la Madiwani leo kwenye ukumbi wa Halmashauri kulia ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga,Daudi Mayeji kushoto ni Naibu Meya wa Jiji hilo,Mohamed Haniu
Mkurugenzi wa Jiji la Tanga,Daudio Mayeji akizungumza katika kikao hicho kushoto ni Mstahiki Meya wa Jiji hilo,Alhaji Mustapa Mhina Selebosi anayefuata ni Naibu Meya Mohamed Haniu na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga,Meja
Naibu Meya Mohamed Haniu akizungumza katika kikao hicho kulia ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaji Mustapha Mhina Selebosi
Waheshimiwa madiwani wa Jiji la Tanga wakifanya dua kabla ya kuanza kikao hicho
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaji Mustapha Mhina Selebosi katika akiwa na Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji kulia na Naibu Mstahiki Meya Mohamed Haniu wakipitia taarifa mbalimbali wakati wa kikao hicho leo

Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaji Mustapha Mhina Selebosi katika akisisitiza jambo kwenye kikao hicho kulia ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji na kushoto ni Naibu Meya wa Jiji la Tanga ,Mohamed Haniu