.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kimataifa. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kimataifa. Onyesha machapisho yote

Jumanne, 3 Aprili 2018

WINNIE MADIKIZELA-MANDELA KUZIKWA APRILI 14

Utawala wa kifalme wa Abathembu umesema unaandaa taratibu za maziko ya mwanaharakati wa kupinga ubaguzi enzi za utawala makaburu nchini Afrika Kusini Winnie Madikizela-Mandela katika eneo la Qunu huko Eastern Cape.

Wakati utawala huo ukitangaza maandalizi hayo Rais wa Afrika Kusini Bw. Cyril Ramaphosa amesema kuwa marehemu, Winnie ambaye anatambulika kwa wengi kama Mama wa Taifa atafanyiwa maziko ya kitaifa tarehe 14 mwezi huu.

Kufanyika kwa maziko ya Mama Winnie Mandela Qunu kunatokana na yeye kuolewa mtu wa kutoka ukoo ya kabila la Abathembu ambaye ni rais wa kwanza mwafrika nchini Afrika Kusini hayati Nelson Mandela kwa miaka 38.

Msemaji wa ufalme wa Abathembu, Prince Siganeko Dalindyebo amesema kuwa familia ya kifalme inaona inaowajibu na kutaka mwili wa Winnie uletwe nyumbani Qunu ambapo atapumzika kwa amani, kwani kwa mujibu wa mila hakuwa amepewa talaka.

Alhamisi, 29 Machi 2018

LET AFRICA EVOLVE, SAYS ZIMBABWEAN PRESIDENT EMMERSON MNANGAGWA AT THE AFRICA CEO FORM

The President of Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa and former President of Nigeria_ Olusegun Obasanjo

ABIDJAN, Ivory Coast, 27th March 2018, -/African Media Agency (AMA)/- Economic recovery and institution building are the challenges faced by all African countries today.

During a panel discussion organised by the Africa CEO Forum around the theme.

When Leaders make History, the President of Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa and former President of Nigeria, Olusegun Obasanjo, shared their experiences on the sustainable and inclusive growth of Africa in general and their own countries in particular.

According to President Emmerson Mnangagwa, Africa's problem is "the failure of leadership". President Mnangagwa continued, saying, "Geographically, my country is far from Nigeria but that did not stop Nigeria from helping us when we needed it. It is this vision that we African leaders should share: mutual aid. Africa needs to learn how to manage its own problems, and this starts with the balance between leadership and institutions". He believes that the executive, the legislature and the judiciary should be independent. Each must perform its mission freely and transparently, but play a complementary role.

The sustainable and inclusive growth sought by African countries is only possible if civil society and elected politicians operate without interference. "We have civilian organisations that come to our countries to support our people by building schools and health centres. It's their role and we welcome that. What we do not accept is that they interfere in our politics. You cannot come from outside and tell us who we need to put at the head of our country, think our politics for us. We must let Africa evolve," he said.

Zimbabwe has begun its economic recovery through the implementation of an agrarian reform process that enabled 367 families to gain access to land.

"We are attempting to evaluate the situation before launching reforms. But we have started land redistribution. This was one of the major problems that we had to solve in Zimbabwe. Today, we need a structure to fight famine and poverty. For now, we are giving our farmers the means to improve and increase production. The food shortage will be alleviated through this system," said President Mnangagwa, who also announced that women and young people will be given a prominent place in national decision-making.

Jeune Afrique Media Group's Publication Director, Marwane Ben Yhamed
In his speech, Nigeria's former president, Olusegun Obasanjo, said that, in the fight against corruption, there was one principle to be respected: that of having strong institutions and effective leadership. "It's good to have a law that sets up a strong institution. But you have to have the men who go with them, effective people. If not, we will not complete our mission. Our goals will never be achieved," he said.

Cost-effective exports and affirmative action for women and young people will also contribute to the success of this highly awaited economic recovery.
The panel discussion ended on these words, after which the Jeune Afrique Media Group's Publication Director, Marwane Ben Yhamed, closed the sixth edition of the Africa CEO forum.

Distributed by African Media Agency (AMA) on behalf of AFRICA CEO FORUM.

Jumatano, 14 Machi 2018

MWANASAYANSI MAARUFU PROFESA STEPHEN HAWAKING AFARIKI DUNIA

Mwanasayansi maarufu duniani bingwa Fizikia Profesa Stephen Hawaking amefariki dunia mapema leo akiwa na umri wa miaka 76.

Familia ya Hawaking ambaye alikuwa ni mtu mwenye maono ya hali ya juu, imesema mwanafizikia huyo amefariki akiwa nyumbani kwake Cambridge.

Mwanasayansi huyo Muingereza alijipatia umaarufu duniani pia anafahamika mno kwa vitabu vyake vya sayansi kikiwemo cha A Brief History of Time.

Akiwa na umri wa miaka 22 Profesa Hawking alipewa miaka michache tu ya kuishi baada ya kubainika kuugua ugonjwa adimu wa nyuroni.

Ijumaa, 2 Machi 2018

BARAFU YAUWA WATU 55 ULAYA NA KULETA MAAFA

                           Mtu akiwa na beleshi akijaribu kuondoa barafu zilizofunika gari lake
Eneo kubwa la Ulaya limeendelea kukabiliwa na hali ya hewa ya barafu huku hali hiyo katika nchi ya Serbia ikiendelea kusababisha madhara.

Barafu nzito imefunika barabara na kukwamisha usafiri wa magari, pamoja na reli na kupelekea pia shule kufungwa huku mamia ya safari za ndege zikihairishwa.

Idadi ya vifo vinavyotokana na hali hiyo mbaya ya hewa vimeongezeka na kufikia watu 55 na majeruhi 21 nchini Poland.

Hali hiyo ya barafu imepelekea Shirika la Afya Duniani (WHO), kusema kuwa masikini, watu wasionamakazi na wahamiaji wataathirika mno na baridi kali.

AL- SHABAAB YAUWA POLISI WATANO KENYA

Polisi watano wameuwawa nchini Kenya na wengine watatu kujeruhiwa katika shambulizi lililofanywa na wapiganaji wa kundi la Al-Shabaab kwenye kambi mbili za usalama katika mji Fino, Kaunti ya Mandera.

Naibu Kamisha wa Polisi wa Kaunti hiyo, Eric Oronyi amesema kuwa shambulizi hilo lililofanywa majira ya saa saba usiku wa kumkia leo lililenga kambi za polisi wa kawaida na wale wa utawala katika mji wa Fino.

Polisi wamesema kuwa washambuliaji hao pia wameharibu mnara wa mawasiliano na kukata kabisa mawasiliano katika eneo hilo.

Kamishna wa polisi Oronyi amesema kuwa washambuliaji wa kundi la Al-Shabaab walikuwa kati ya 70 hadi 100 walivamia wakija kwa miguu.

Alhamisi, 1 Machi 2018

MAKANISA 700 YAFUNGWA NCHINI RWANDA KWA KELELE

Serikali ya Rwanda imeyafunga makanisa yapatayo 700 kwa kushindwa kukidhi vigezo vya majengo na kwa kusababisha kelele.

Taarifa ya Shirika la Habari la BBC, inasema mengi ya makanisa yaliyofungwa nchini Rwanda ni makanisa madogo ya dhehebu la Kipendekosti pamoja na msikiti mmoja.

Afisa mmoja wa serikali amesema kuwa zaidi ya majengo 700 ya kanisa yaliyofungwa yameshafunguliwa baada ya kukidhi vigezo na kuridhiwa na wakaguzi.

Kwa mujibu wa mapendekezo ya sheria mpya, wahubiri wote wanapaswa kuwa wamepata mafunzo ya thiolojia kabla ya kuanzisha kanisa.

Makanisa ya Kipentekosti ambayo yamekuwa yakiendeshwa na wahubiri wanaodai kuwa na uwezo wa kufanya miujiza yamekuwa yakiongezeka katika maeneo mengi ya Afrika katika miaka ya hivi karibuni.

Alhamisi, 15 Februari 2018

WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA AJIUZULU

        Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn ( pichani ) amejiuzulu 

Taarifa zilizotangazwa na kituo cha televiseheni cha taifa hilo zimesema kuwa Waziri Mkuu huyo pia amewasilisha barua yake ya kujiuzulu Uenyekiti wa chama chake cha Ethiopia People's Demecratic front.

Pamoja na kwamba hakuna sababu rasmi zilizotolewa za kujiuzulu kwa Desalegn, habari za uhakika zinasema kuwa uhenda ni kufuatia kuepusha mgogoro wa kisiasa zaidi nchini humo ambapo kumekuwa na maandamano dhidi ya serikali katika maeneo yenye makabila makubwa nchini humo ya Oromia na Amhara.

Watu 10 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika maandamano ya upinzani.

Hailemariam Desalegn aliingia madarakani Agosti 2012, baada ya kufariki kwa kiongozi shupavu Meles Zenawi.

Uchumi wa Ethiopia umekuwa ukikua kwa kasi, na hatua hii ya Desalegn inatishia mustakabali wa baadaye wa taifa hilo

WAZIMBABWE WAOMBOLEZA KIFO CHA MORGAN TSVANGIRAI

Wananchi wa Zimbabwe wanaomboleza kifo cha aliyewahi kuwa Waziri Mkuu na kiongozi wa upinzani wa chama cha siasa cha MDC Bw. Morgan Tsvangirai.

Bw. Tsvangirai alifariki dunia jana huko Johannesburg nchini Afrika Kusini akiwa na umri wa miaka 65 akisumbuliwa na saratani ya utumbo.

Tsvangirai alibainika kusumbuliwa na ugonjwa huo mwaka 2016 na alikuwa akifanyiwa matibabu ya mara kwa mara katika kituo cha matibabu cha Donald Gordon huko Parktown.

Jumanne, 13 Februari 2018

MWANASHERIA MKUU WA KENYA, GITHU MUIGAI AJIUZULU

Mwanasheria mkuu wa Kenya, Githu Muigai amejiuzulu. 

Taarifa kutoka Kenya zinasema kuwa tayari Rais wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta amemteua Jaji Paul Kihara Kariuki kuwa mwanasheria mkuu

Alhamisi, 8 Februari 2018

MIGUNA MIGUNA ADAI POLISI KENYA WALIMFANYIA UNYAMA

Mwanasheria machachari nchini Kenya Miguna Miguna ameeleza kuwa alikuwa akifanyiwa mambo ya kinyama akiwa mikononi mwa polisi katika siku tano alizoshikiliwa.

Katika mahojiano na Shirika la BBC huko Amsterdam akiwa njiani kuelekea Canada, Miguna aliyefukuzwa Kenya juzi, amesema alipelekwa katika vituo sita vya polisi.

Miguna alikamatwa Februari 2, nyumbani kwake Runda Jijini Nairobi na polisi wapatao 30, akikabiliwa na tuhuma za kumuapisha Raila Odinga na kujitanga Jenerali wa kundi la lililopigwa marufuku la NRM.

Jumatatu, 5 Februari 2018

RAIS JACOB ZUMA AKABILIWA NA SHINIKIZO LA KUJIUZULU

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma anakabiliwa na shinikizo la kumtaka ang'atuke katika madaraka ya urais.

Rais Zuma na wanachama waandamizi wa chama cha African National Congress (ANC) walifanya mazunguzo jana, na hii leo viongozi wa chama hicho waliitisha mkutano wa dharura.

Vyombo vya habari vya Afrika Kusini vimeripoti kuwa rais Zuma amekaidi shinikizo la chama chake na kugoma kujiuzulu urais, lakini taarifa rasmi za mkutano huo bado hazijatolewa.

Rais Zuma ambaye anakabiliwa na tuhuma za rushwa, nafasi yake ya uongozi wa ANC ilichukuliwa na Cyril Ramaphosa mwezi Desemba.

MCHUNGUZI WA MATUKIO YA UJANGILI AUWAWA NCHINI KENYA

Mmoja wa wachunguzi mahiri wa matukio ujangili Esmond Bradley Martin amekutwa akiwa amekufa nyumbani kwake eneo la Karen Jijini Nairobi nchini Kenya.

Esmond ambaye ametumia miongo kadhaa kuongea na wafanyabiashara, wasafirishaji kwa magedo nyara za serikali katika kuchunguza njia za magendo duniani amekufa katika mazingira ya kutatanisha.

Mjumbe huyo wa Umoja wa Mataifa wa kuwalinda Faru amekutwa akiwa na majeraha ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali shingo.

Edmond mwenye miaka 75, amekuwa mstari wa mbele kupigana na ujangili, na kuandika chunguzi nyingi za taarifa ya magendo ya faru na tembo nchini Kenya na biashara yake katika nchi za Asia.

Jumapili, 28 Januari 2018

WAKAZI WA MJI WA CAPE TOWN WATAKIWA KUBANA MATUMIZI YA MAJI

Wakazi wa Mji wa Cape Town nchini Afrika Kusini wametakiwa kuhifadhi maji kama vile maisha yao yanategemea maji, ili kuepusha kufungwa kwa huduma ya maji.

Ukame mkali umelazimisha Manispaa ya Jiji hilo kudhibiti matumizi kufikia lita 50 sawa na galoni 11 kwa mtu mmoja kwa siku.

Maafisa wa Jiji la Cape Town wamewasihi watu kuacha kutumia maji ya kuflash chooni, ili kuhifadhi maji.

Mkuu wa serikali ya Mkoa wa Cape Town amesema kuwa iwapo mabomba yatakosa maji itakuwa ni janga juu ya janga.
   Wakazi wa Jiji la Cape Town wakiwa kwenye foleni ya maji baada ya maji kuadimika
   Wakazi wa Jiji la Cape Town wakiwa na madumu wakihaha kutafuta maji yaliyoadimika

Ijumaa, 19 Januari 2018

MKUTANO MKUU WA KUIFUFUA UPYA JUMUIYA YA WATANZANIA DMV

Watanzania waishio Washington DC na Vitongoji vyake, siku ya Jumapili Jan 14, waliweza kufanya maamuzi ya kuifufua tena Jumuiya ya Watanzania DMV, ilivunjika kwa zaidi ya miaka miwili hadi kufikia kufanya maamuzi ya kuifufua tena upya Jumuiya hiyo.

Kamati ya Maandalizi pamoja na waTanzania waliohudhuria katika mkutano huo, waliweza kufanya maamuzi ya kuteuwa watu saba kuwa ndani ya Kamati ya Uchaguzi, ili kushindikiza katika uchaguzi kujachua viongozi wapya watakaojitokeza kuchukua fumu za kugombea uongozi wa Jumuiya hiyo.

Viongozi wa Kamati ya Mda ya Uchaguzi waliochaguliwa na Watanzania waliohudhuria katika mkutano huo ni ; Robert Saulanga - Mwenyekiti Richard Mawenya - M/Kiti Msaidizi Julius Manase - Katibu Eddha Ghachuma - Muweka Hazina Mama Mushala - Mjumbe Kenyatta - Mjumbe Simba Sakapala - Mjumbe.

                                                  https://www.youtube.com/embed/qllt_Z70cBQ

Ijumaa, 12 Januari 2018

WANAFUNZI WA KIKE GHANA WAKATAZWA KUVUKA MTO WAKIWA KWENYE HEDHI

Wanafunzi wa kike wa shule nchini Ghana wamepigwa marufuku kuvuka mto wakiwa katika siku zao za hedhi pamoja na katika siku za jumanne.

Marufuku hiyo iliyotolewa na mungu wa mto huo, imewakasirisha wanaharakati, kutokana na kuwa wasichana lazima wavuke mto ili kwenda shule.

Hii inamaana kuwa wasichana katika Wilaya ya Upper Denkyira Mashariki, katika Mkoa wa Kati, watakosa masomo wakiwa kwenye hedhi na siku za jumanne.

Alhamisi, 11 Januari 2018

KENYA AIRWAYS STARTS TICKET SALES FOR ITS NON - STOP DAILY FLIGHT TO NEW YORK

NAIROBI, Kenya, January 11, 2018/ -- Kenya Airways (www.Kenya-Airways.com) today marks a great milestone with the launch of a non-stop flight from Nairobi to New York. The national carrier starts selling today tickets for the inaugural flight which is scheduled for October 28th this year.

Copyright free broadcast-quality footage, pre-recorded interviews, shot list and dope sheet are available for media to download here: http://APO.af/n5xQtN

Kenya Airways becomes the first airline to offer a non-stop flight between East Africa and the United States of America.

The airline already serves Africa, Europe, Middle-East, Indian sub-continent and Asia. The opening of the US destination completes an essential piece for Kenya Airways’ network, cementing its position as one of the leading African carriers.

“This is an exciting moment for us. It fits within our strategy to attract corporate and high-end tourism traffic from the world to Kenya and Africa. We are honored to contribute to the economic growth of Kenya and East Africa.” said Kenya Airways Group Managing Director and CEO Sebastian Mikosz.

With over 40 American multinationals located in Nairobi and many more across Africa, the launch of daily flights is expected to further spur trade between America and Africa.

Kenya Airways will offer its customers a unique travel experience between two great gateways. It will be the fastest connection from East Africa to New York, with a 15 hours duration eastbound and 14 hours westbound. The ultra-long-haul flight, unique to Kenya Airways network, will require 4 Pilots and 12 Flight attendants as well as 85 tons of fuel each way, making it an exceptional operation.

The airline will operate its state of the art Boeing 787 Dreamliner with a capacity of 234 passengers. The flight will depart every day from Jomo Kenyatta International Airport hub in Nairobi at 23:25 arriving at JFK airport in New York at 06:25 the following day. From New-York it will depart at 12:25 landing at JKIA at 10:55 the following day. Its duration will be 15 hours east bound and 14 hours west bound.

This convenient schedule will allow connections to and from over 40 African destinations through Kenya Airways hub in Nairobi.
Distributed by APO Group on behalf of Kenya Airways.

Jumapili, 31 Desemba 2017

BASI LAGONGANA NA LORI KENYA NA KUUWA WATU 36

Watu wapatao 36 wamekufa katika ajali ya barabarani baada ya basi lililojaa abiria likielekea Nairobi kugongana na lori katika eneo la Migaa katika barabara kuu ya Nakuru-Eldoret.

Miongoni mwa waliokufa ni pamoja na dereva wa lori pamoja na utingo wake ambao lori lao lilikuwa linaelekea Eldoret, ambapo miili 28 ya watu waliokufa papo hapo imetolewa kwenye eneo la ajali hiyo mbaya.

Watu 30 wameripotiwa kufa papo hapo na wengine wanne walifariki duniani baadaye wakipatiwa matibabu ya majeraha yao kwenye hospitali ya Nakuru Level Five.

Miongoni mwa wanne waliokufa hospitali ni watoto watatu wenye umri wa miezi miwili, mtoto wa miaka miwili mmoja na wa miaka 10 mmoja pamoja na mtu mzima mwenye umri wa miaka 35.

Jumatatu, 25 Desemba 2017

PAPA AWATAKA WAKATOLIKI KUGUSWA NA MAGUMU YA WAHAMIAJI

Papa Francis amewataka Wakatoliki kutilia maanani magumu wanayopitia wahamiaji waliokimbia nchi zao, kauli ambayo ametoa katika misa ya mkesha wa Krismasi.

Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki Duniani amelinganisha mateso ya wahamiaji na Maria na Joseph, ambao Biblia inaelezwa walisafiri kutoka Nazareth kwenda Bethlehem na kukosa sehemu ya kukaa.

Papa ambaye hii leo anatarajiwa kutoa hotuba yake ya Krismasi kwa miji na dunia, amesema anatumia mamlaka yake ya kiroho kuwaombi ulinzi wahamiaji.

KUACHIWA KWA MSAMAHA FUJIMORI KWAIBUA MAANDAMANO PERU

Rais wa Peru Pedro Pablo Kuczynski amemuachia kwa msamaha kiongozi wa zamani wa nchi hiyo Alberto Fujimori kutokana na kutokuwa na afya njema, jambo ambalo limeibua maandamano ya kupinga.

Fujimori mwenye miaka 79, ambaye alikuwa anatumikia kifungo cha miaka 25 kwa kukiuka haki za binadamu pamoja na rushwa, aliondolewa kutoka gerezani na kuhamishiwa hospitali baada ya kuugua jumamosi.

Rais Kuczynski amekanusha hatua yake hiyo ya kutoa msamaha kwa Fujimori ni sehemu ya makubaliano na chama chake waliyofikia wiki iliyopita ili kumuepusha naye asichukuliwe hatua za kumuadhibu.

Jumatano, 20 Desemba 2017

AL-MALIKI: NCHI WANACHAMA WA BARAZA LA USALAMA, ZAUNGANA KUPINGA AZIMIO LA MAREKANI

Nchi 14 wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, zimeunga mkono rasimu ya azimio iliyowakilishwa na Misri kwa niaba ya Palestina, inayotaka kutupiliwa mbali azimio la Rais wa Marekani “Donald Trump”, linaloitambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israeli, huku Marekani pekee ikiipinga rasimu hiyo na kutumia kura ya veto ili kuifelisha, baada ya kugundua ya kwamba inaungwa mkono na nchi hizo.

Kwa upande wake, Dk.Riyad Al-Maliki ambae ni Waziri wa Mambo ya Nje na Wahamiaji wa Palestina, ametia mkazo kwamba kura ya pmoja ya nchi wanachama wa Baraza la Usalama, Marekani imejikuta ikibaki pekee katika suala la misingi ya sheria za kimataifa na maazimio ya jumuiya ya kimataifa.

Maliki alisema ni fursa kwa Marekani kuachana na uamuzi wake ulio kinyume cha sheria na kurudi kwenye kushikamana na Mkataba, sheria na matakwa ya kimataifa, lakini kwa masikitiko imechagua kusimama katika upande mbaya wa historia, upendeleo wa ukoloni, udhalimu na kudhoofisha juhudi zote za amani katika Mashariki ya Kati na ulimwengu mzima.

Aidha, ameitaka Marekani kufuta uamuzi wake, akitilia mkazo kwamba kutumia kura ya veto hakumlindi na majukumu yake, ambayo ni ukiukaji mpya wa misingi iliyosimamishiwa Umoja wa Mataifa, kukiuka mikataba na matendo ya taasisi zake.

Na kwamba kura hiyo ya veto, hata kama haitobadili chochote katika hali na hadhi ya Jerusalemu kama mji mkuu wa Palestina inayokaliwa kimabavu, lakini bila shaka yoyote itabadili nafasi ya Marekani kama mpatanishi wa mchakato wa amani na mchakato mwingine wowote wa kisiasa ujao.

Maliki ameongeza kusema kuwa, kujilinda kwa nchi kupo katika kuheshimu sheria za kimataifa, sio kutoa kinga na kuwezesha Mataifa yanayokiuka na kufanya uhalifu ili kuepuka kuadhibiwa, kama ilivyo sasa na Israeli yenye utawala wa kivamizi na kimabavu.

Maliki ametia mkazo kuwa, haki ya suala la Palestina, kusimama kidete wananchi wetu na kujitolea muhanga, pia kuthibiti kwa uongozi wa Palestina katika kanuni ya kimaadili, na kuheshimu kwake misingi ya sheria za kimataifa katika kukabili uvamizi wa kikoloni na wa kimakazi, limekuwa ni suala la makubaliano ya kimataifa na kubwa zaidi kuliko kuzingatia mahesabu na masilahi madogo ya serikali hii au ile. Vilevile uingiliaji wowote katika suala hili kutoka upande wowte, ni kupunguza uaminifu wa upande huo.

Waziri wa Mambo ya Nje pia amezishukuru nchi zilizopigia kura ya ndio azimio hilo na zile nchi zilizosimama upande wa misingi yake katika haki, uadilifu na sheria za kimataifa, ambazo moja kwa moja zinaelekea katika masilahi ya taifa la Palestina na suala lake,kwa sababu Jerusalem ndio moyo ulio hai wa Palestina na ndio funguo ya amani na msingi wake.


Kwa kumalizia, Maliki ameahidi kuendeleza juhudi ili kutekeleza mpango wa uongozi wa Palestina uliomo katika hotuba ya Mheshimiwa Rais, aliyoitoa katika mkutano wa dharura ya Kiislamu katika kuilinda Jerusalem na Wananchi wetu wa Palestina, ili kufikia kukomesha uvamizi wa kimabavu na kufikia haki za msingi za Palestina, vile vile kusimamisha dola ya Palestina yenye mji mkuu wake Jerusalem, huku wakimbizi wakipalestina wakirejea nyumbani walikofukuzwa kwa nguvu,hayo yote ni kwa mujibu wa azimio namba 194.