Mtu akiwa na beleshi akijaribu kuondoa barafu zilizofunika gari lake
Eneo kubwa la Ulaya limeendelea
kukabiliwa na hali ya hewa ya barafu huku hali hiyo katika nchi ya
Serbia ikiendelea kusababisha madhara.
Barafu nzito imefunika barabara na
kukwamisha usafiri wa magari, pamoja na reli na kupelekea pia shule
kufungwa huku mamia ya safari za ndege zikihairishwa.
Idadi ya vifo vinavyotokana na hali
hiyo mbaya ya hewa vimeongezeka na kufikia watu 55 na majeruhi 21
nchini Poland.
Hali hiyo ya barafu imepelekea
Shirika la Afya Duniani (WHO), kusema kuwa masikini, watu
wasionamakazi na wahamiaji wataathirika mno na baridi kali.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni