Polisi watano wameuwawa nchini Kenya
na wengine watatu kujeruhiwa katika shambulizi lililofanywa na
wapiganaji wa kundi la Al-Shabaab kwenye kambi mbili za usalama
katika mji Fino, Kaunti ya Mandera.
Naibu Kamisha wa Polisi wa Kaunti
hiyo, Eric Oronyi amesema kuwa shambulizi hilo lililofanywa majira ya
saa saba usiku wa kumkia leo lililenga kambi za polisi wa kawaida na
wale wa utawala katika mji wa Fino.
Polisi wamesema kuwa washambuliaji
hao pia wameharibu mnara wa mawasiliano na kukata kabisa mawasiliano
katika eneo hilo.
Kamishna wa polisi Oronyi amesema
kuwa washambuliaji wa kundi la Al-Shabaab walikuwa kati ya 70 hadi
100 walivamia wakija kwa miguu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni