Mwanasayansi maarufu duniani bingwa
Fizikia Profesa Stephen Hawaking amefariki dunia mapema leo akiwa na
umri wa miaka 76.
Familia ya Hawaking ambaye alikuwa
ni mtu mwenye maono ya hali ya juu, imesema mwanafizikia huyo
amefariki akiwa nyumbani kwake Cambridge.
Mwanasayansi huyo Muingereza
alijipatia umaarufu duniani pia anafahamika mno kwa vitabu vyake vya
sayansi kikiwemo cha A Brief History of Time.
Akiwa na umri wa miaka 22 Profesa
Hawking alipewa miaka michache tu ya kuishi baada ya kubainika kuugua
ugonjwa adimu wa nyuroni.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni