Wananchi wa Zimbabwe wanaomboleza
kifo cha aliyewahi kuwa Waziri Mkuu na kiongozi wa upinzani wa chama
cha siasa cha MDC Bw. Morgan Tsvangirai.
Bw. Tsvangirai alifariki dunia jana
huko Johannesburg nchini Afrika Kusini akiwa na umri wa miaka 65
akisumbuliwa na saratani ya utumbo.
Tsvangirai alibainika kusumbuliwa na
ugonjwa huo mwaka 2016 na alikuwa akifanyiwa matibabu ya mara kwa
mara katika kituo cha matibabu cha Donald Gordon huko Parktown.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni