.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 5 Februari 2018

MCHUNGUZI WA MATUKIO YA UJANGILI AUWAWA NCHINI KENYA

Mmoja wa wachunguzi mahiri wa matukio ujangili Esmond Bradley Martin amekutwa akiwa amekufa nyumbani kwake eneo la Karen Jijini Nairobi nchini Kenya.

Esmond ambaye ametumia miongo kadhaa kuongea na wafanyabiashara, wasafirishaji kwa magedo nyara za serikali katika kuchunguza njia za magendo duniani amekufa katika mazingira ya kutatanisha.

Mjumbe huyo wa Umoja wa Mataifa wa kuwalinda Faru amekutwa akiwa na majeraha ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali shingo.

Edmond mwenye miaka 75, amekuwa mstari wa mbele kupigana na ujangili, na kuandika chunguzi nyingi za taarifa ya magendo ya faru na tembo nchini Kenya na biashara yake katika nchi za Asia.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni