Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma
anakabiliwa na shinikizo la kumtaka ang'atuke katika madaraka ya
urais.
Rais Zuma na wanachama waandamizi wa
chama cha African National Congress (ANC) walifanya mazunguzo jana,
na hii leo viongozi wa chama hicho waliitisha mkutano wa dharura.
Vyombo vya habari vya Afrika Kusini
vimeripoti kuwa rais Zuma amekaidi shinikizo la chama chake na kugoma
kujiuzulu urais, lakini taarifa rasmi za mkutano huo bado
hazijatolewa.
Rais Zuma ambaye anakabiliwa na
tuhuma za rushwa, nafasi yake ya uongozi wa ANC ilichukuliwa na Cyril
Ramaphosa mwezi Desemba.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni