Serikali ya Rwanda imeyafunga
makanisa yapatayo 700 kwa kushindwa kukidhi vigezo vya majengo na kwa
kusababisha kelele.
Taarifa ya Shirika la Habari la BBC,
inasema mengi ya makanisa yaliyofungwa nchini Rwanda ni makanisa
madogo ya dhehebu la Kipendekosti pamoja na msikiti mmoja.
Afisa mmoja wa serikali amesema kuwa
zaidi ya majengo 700 ya kanisa yaliyofungwa yameshafunguliwa baada ya
kukidhi vigezo na kuridhiwa na wakaguzi.
Kwa mujibu wa mapendekezo ya sheria
mpya, wahubiri wote wanapaswa kuwa wamepata mafunzo ya thiolojia
kabla ya kuanzisha kanisa.
Makanisa ya Kipentekosti ambayo
yamekuwa yakiendeshwa na wahubiri wanaodai kuwa na uwezo wa kufanya
miujiza yamekuwa yakiongezeka katika maeneo mengi ya Afrika katika
miaka ya hivi karibuni.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni