Ni Katibu wa CCM Wilaya ya Hanang,
Mkoani Manyara,Teddy Athumani (wa kwanza kutoka kulia) akipitia
makabrasha ya mkutano wa baraza la madiwani wa Halmashauri ya wilaya
ya Hanang kujiridhisha namna watendaji wa Halmashauri wanavyotekeleza
ilani ya chama tawala.
Ni Mbunge wa jimbo la Hanang, Mkoani
Manyara, Dk.Mary Nagu (wa pili kutoka kulia) akipitia taarifa ya
utoaji mikopo kwa vikundi vya wanawake,vijana na walemavu
iliyowasilishwa kwenye mkutano huo na kisha kutaka kufahami shilingi
milioni 300 zilizoagizwa kwenye mkutano wa LAC Dodoma zitalipwa lini
ili vikundi vya wanawake,vijana na walemavu viweze kunufaika na
kujiongezea mitaji yao.
Ni Mkuu wa wilaya ya Hanang, Sara
Msafiri akisisitiza jambo kwenye mkutano wa baraza la madiwani wa
Halmashauri ya wilaya ya Hanang uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano
wa Halmashauri hiyo.
Ni Katibu wa vikao vya Halmashauri
ya wilaya ya Hanang ,Stevine Yonah (wa kwanza kutoka kushoto) akinukuu
maazimio yote ya mkutano wa Baraza hilo ili watendaji waweze
kutekeleza kikamilifu maazimio hayo.(Picha zote Na Jumbe Ismailly)
Na. Jumbe Ismailly HANANG
Machi,01,2018 Mazingira
KUTOKANA na hali ya uharibifu wa
misitu katika wilaya ya Hanang kuwa kubwa sana,Mkuu wa wilaya ya
Hanang,Mkoani Manyara,Sara Msafiri ameziagiza kamati za maendeleo za
kata kujenga utamaduni wa kujadili katika vikao vyao juu ya hali ya
uhifadhi wa misitu katika maeneo yao.
Akitoa agizo hilo kwenye mkutano wa
kawaida wa Baraza la kawaida la madiwani wa Halmashauri hiyo,Mkuu wa
wilaya huyo aliyataja baadhi ya maeneo ya vijiji vya Lalaji.Balangida
na maeneo mengine hali ya mazingira ni mbaya sana.
“Kwa hiyo niwaombe kwamba kamati
za maendeleo za kata mjadili na hali ya hifadhi ya misitu na ninazo
taarifa za kutosha na nimejirisha wapo viongozi wengine ni wa
kisiasa wanashiriki katika biashara ya kukata miti,kuchoma na kuuza
mkaa.”alisisitiza Mkuu huyo wa wilaya.
Kwa mujibu wa Mkuu wa wilaya kupitia
serikali kuu wameshatoa maagizo kwa watendaji kwamba mtu yeyote tule
atakayetaka kukata miti hata kama aliupanda mwenyewe ni lazima apate
kibali kutoka kwa Mkuu wa wilaya.
Hata hivyo Sara alisisitiza kwamba
ni ukweli usiopingika na alioufanyia uchunguzi wa kina na
kujiridhisha kuwa kuna baadhi ya viongozi wa kisiasa,wakiwemo
madiwani,wenyeviti wa vijiji,vitongoji na watendaji wanajihusisha na
biashara ya kukata micti kuchoma mkaa na kuuza mazao hayo.
Akimpongeza Mkuu huyo wa
wilaya,Mbunge wa jimbo la Hanang,Dk.Mary Nagu pamoja na kumpongeza
Mkuu wa wilaya kwa jitihada zake za kulinda naa kuhifadhi
mazingira,lakini aliweka bayana kuwa kama kuna jambo ambalo haliendi
vizzuri katika wilaya hiyo ni suala la mazingira.
Diwani wa kata ya Hanang,mjini Peter
Lori alionyesha kutoridhishwa na namna Halmashauri isivyoujali msitu
wa hifadhi wa Mreru kwani kwa kipindi kirefu serikali imeitelekeza
hifadhi hiyo.
Hata hivyo diwani huyo alifafanua
pia kwamba inasemekana hifadhi hiyo ni mapito ya wanyama na kuhoji
kwamba ni lini Mkuu wa wilaya hiyo atafikiria msitu wa hifadhi Mreru
utakuwa hifadhi ya Halmashauri ya wilaya hiyo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni