Mwanasheria machachari nchini Kenya
Miguna Miguna ameeleza kuwa alikuwa akifanyiwa mambo ya kinyama akiwa
mikononi mwa polisi katika siku tano alizoshikiliwa.
Katika mahojiano na Shirika la BBC
huko Amsterdam akiwa njiani kuelekea Canada, Miguna aliyefukuzwa
Kenya juzi, amesema alipelekwa katika vituo sita vya polisi.
Miguna alikamatwa Februari 2,
nyumbani kwake Runda Jijini Nairobi na polisi wapatao 30, akikabiliwa
na tuhuma za kumuapisha Raila Odinga na kujitanga Jenerali wa kundi
la lililopigwa marufuku la NRM.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni