Tottenham Hotspur imetinga raundi ya
tano ya michuano ya Kombe la FA kwa kupata ushindi kirahisi wa magoli
2-0 dhidi ya timu ya daraja la pili ya Newport County katika dimba la
Wembley.
Spurs ilimuhitaji Harry Kane kufunga
goli la kusawazisha katika dakika za mwisho na kutoka sare ya 1-1
katika mchezo wa kwanza, haikuonekana kukabiliwa na ushindani katika
mchezo wa jana.
Magoli ya Tottenham yalifungwa na
Dan Butler aliyejifunga wakati akijaribu kuzuia krosi ya Moussa
Sissoko na kisha Erik Lamela akaihakikishia ushindi kwa kufunga goli
la pili.
Dan Butler akionekana kutahayari baada ya kujikuta akifunga kwenye goli lake
Mshambuliaji nyota wa Spur akifuatilia mchezo huo akiwa benchi baada ya kupumzishwa yeye na Christian Eriksen
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni