NA SAMIA CHANDE, SUMBAWANGA
KITUO cha kufua umeme mkoani Rukwa kimepata jenereta ya kufua umeme yenye uwezo wakuzalisha MegawatI 10 zitakazoimarisha uzalishaji wa umeme mkoani humo.
Akizungumzia ujio wa jenereta hiyo, Meneja wa TANESCO Mkoani Rukwa Bw.Herini Muhina, alisema, hali ya uzalishaji umeme itakuwa bora zaidi na hivyo kufanya upatikanaji wa umeme katika wilaya za Sumbawanga, Laila, Kalambo na Nkasi kuwa bora zaidi.
“Nimatumaini yetu kuwa ongezeko hilo la umeme, litasaidia kwenda sambamba na mipango ya serikali ya kujenga uchumi wa viwanda kwani umeme wa uhakika utakuwepo na hivyo kufanya Mkoa wa Rukwa kuwa sehemu nzuri ya kuwekeza kwenye sekta hiyo ya viwanda.” Alitoa hakikisho Bw. Muhidin.
Bw. Daimon akipewa maelezo zaidi ya uendeshaji shughuli za TANESCO mkoani Rukwa. |
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni