Papa Francis amewataka Wakatoliki
kutilia maanani magumu wanayopitia wahamiaji waliokimbia nchi zao,
kauli ambayo ametoa katika misa ya mkesha wa Krismasi.
Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki
Duniani amelinganisha mateso ya wahamiaji na Maria na Joseph, ambao
Biblia inaelezwa walisafiri kutoka Nazareth kwenda Bethlehem na
kukosa sehemu ya kukaa.
Papa ambaye hii leo anatarajiwa
kutoa hotuba yake ya Krismasi kwa miji na dunia, amesema anatumia
mamlaka yake ya kiroho kuwaombi ulinzi wahamiaji.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni