Malaysia kwa kushirikiana na mataifa mengine wanaendelea na uchunguzi mkali wa kuitafuta ndege ya Shirika la ndege la Malaysia iliyopotea ikiwa angani masaa mawili tu baada ya kuondoka Kuala Lumpar kuelekea Beijing China.
Mkuu wa Mamlaka ya Anga wa Malaysia amesema hatma ya ndege ya shirika la ndege la nchi hiyo iliyopotea ni utata usio na jawabu.
Bw. Azharuddin Abdul Rahman amesema maafisa hawajaondoa uwezekano wa ndege hiyo kuwa imetekwa kama sababu ya ndege hiyo kutoweka.
Ndege hiyo ya Shirika la Ndege la Malaysia namba MH370 imepotea karibu siku mbili sasa wakati ikiwa njiani kwenda Beijing ikitokea Kuala Lumpur ikiwa na abiria 239.
Taarifa zinasema ndege hiyo ilipoteza mawasiliano ikiwa katika anga la Malaysia na Vietnam ikiwa na idadi hiyo ya abiria, huku uraia wa abiria wawili ukiwa na utata
Meli, ndege za kijeshi la helkopta zimekuwa zikitumika kuitafuta ndege hiyo toka juzi jumamosi, lakini mpaka sasa hakuna mabaki yoyete ya ndege hiyo kuonekana bahari, hali ambayo bado inaiwia vigumu Malaysia kutangaza kuanguka kwa ndege hiyo




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni