Jumatatu, 10 Machi 2014

WAHAMIAJI HARAMU 42 WAFARIKI, NI BAADA YA BOTI YAO KUZAMA BAHARINI HUKO YEMEN

Wahamiaji 42 kutoka Afrika wamekufa maji nchi ni Yemen baada ya boti yao waliyokuwa wakiitumia kusafiria kuzama baharini kati Pwani ya kusini mwa nchi hiyo.

Wizara ya ulinzi nchini Yemen imesema kuwa mashua hiyo iliyokuwa ikisafirisha wahamiaji haramu, ilizama katika mkoa wa Kusini wa Shabwa, eneo ambako maelfu ya wahamiaji wa kutoka Afrika huwasili kila mwaka.

Meli za wanamaji wa Yemen zinazofanya doria baharini zimewaokoa watu 30 ambao wamepelekwa kuhifadhiwa kambi ya wakimbizi katika mji wa Mayfaa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni