Jumatano, 12 Machi 2014

KLABU BINGWA ULAYA, USIKU WA LEO NI FC BARCELONA NA MANCHESTER CITY

 Aguero, Nasri na Yaya Toure wa Manchester City wakijifua kabla ya mchezo wa ligi ya mabingwa usiku wa leo dhidi ya wenyeji wao Barcelona.

Usiku wa leo ni kizaa zaa nguo kuchani katika mchezo wa marudiano wa klabu bingwa barani Ulaya, pale Barcelona watakaposhuka dimbani kucheza na Manchester City huku wakiwa na faida ya kushinda 2-0 katika mchezo wa awali uliochezwa Etihad Stadium.

Barcelona wana nafasi kubwa ya kusonga mbele hatua ya robo fainali kutokana na ukweli kwamba ni vigumu labda kwa miujiza Man City wawafunge mabao 3-0 leo usiku.
Uwanja wa Nou Camp ambao utatumiwa usiku wa leo katika mchezo wa marudianio hatua ya 16 bora ligi ya mabingwa Ulaya kati ya Barcelona na Manchester City 
                          Neymar wa Fc Barcelona akijifua kabla ya mpambano huo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni