Rweyunga Blog

Jumamosi, 15 Machi 2014

KUELEKEA UCHAGUZI KESHO JIMBO LA KALENGA, KATIBU MKUU CCM KINANA AMNADI GODFREY MGIMWA KWA WANANCHI

Mgombea Ubunge Jimbo la Kalenga kwa tiketi ya CCM,Ndugu Godfreya Mgimwa akijinadi kwa wakazi wa kijiji cha Magulilwa,kata ya Magulilwa Iringa Vijijini wakati wa mkutano wa kampeni  za lala salama,amapo uchaguzi unatarajiwa kufanyika Machi 16,siku ya jumapili.
 Wananchi waliojazana katika mkutano huo wakishangilia baada ya kusikia sera za mgombea
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana pichani kushoto na Naibu Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Mwigulu Nchemba wakimnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga kupitia chama hicho cha CCM,Ndugu Godfreya Mgimwa,kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za lala salama,uliofanyika leo jioni katika kijiji cha Magulilwa kata ya Magulilwa,Iringa vijijini.
 Katibu Mkuu wa CCm,Ndugu Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Magulilwa mapema leo jioni wakati wa mkutano wa kampeni za lala salama,alipokuwa akimnadi mgombea Ubunge kupitia chama hicho,Ndugu Godfreya Mgimwa kwa wananchi.


at 07:28
Shiriki

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

‹
›
Nyumbani
Ona toleo la wavuti
Inaendeshwa na Blogger.