Matajiri wa jiji la London, Chelsea hii leo wameendelea kujiimarisha kileleni katika msimamo wa ligi kuu Uingereza baada ya kuiangamiza Tottenham kwa mabao 4-0 katika mchezo ulioshuhudia vijana hao wa kocha msema hovyo Jose Mourinho wakiutumia vyeam uwanja wao wa nyumbani.
Chelsea walijipatia mabao yao kupitia kwa Samuel Eto'o dakika ya 56, Eden Hazard dakika ya 60 kwa mkwaju safi wa penati na mtokea benchi Demba Ba akifunga mara mbili kunako dakika ya 88 na 89. Kwa matokeo hayo Chelsea wana pointi 66 na kuendelea kuongoza ligi kuu Uingereza wakifuatiwa na Liverpool walio nafasi ya pili na point 59
Eto'o akiambaa ambaa uwanjani baada ya kuifungia timu yake bao
Kaka chagua uende wewe au mpira, lakini mmoja abaki hapa
Younes Kabul wa Tottenham akizawadiwa kadi nyekundu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni