Jumamosi, 8 Machi 2014

LIGI KUU UINGEREZA, MAN U YAICHAPA WEST BROM 3-0

 Ligi kuu ya Uingereza imeendelea hii leo kwa kushuhudia Manchester United ikiibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya West Brom katika mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa. Mabao ya mashetani wekundu ambao leo wamewapa raha mashabiki wao yalifungwa na Wayne Rooney, Phil Jones na Danny Welbeck. Kwa matokeo hayo Man United ipo nafasi ya sita katika msimamo wa ligi kuu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni