Ndege ya shirika la ndege la Malaysia Boeing 777 iliyokuwa na abiria 239 imepoteza mawasiliano ikiwa inatokea Kuala Lumpar Malaysia kuelekea Beijing China. Abiria waliokuwa ndani ya ndege hiyo ni kutoka Marekani, Australia, Ufaransa na China. Hakuna taarifa zaidi ya kupoteza mawasiliano kwa ndege hiyo kwamba imeanguka au la, na uchunguzi zaidi unaendelea
Mmoja wa jamaa aliyefika uwanjani hapo akisoma tangazo la kutua na kupaa kwa ndege
Ndugu waliokuwa wanawasubiri jamaa zao waliosafiri na ndege hiyo wakilia baada ya kusikia tangazo kuwa hakuna mawasiliano kati ya uwanjani hapo na ndege hiyo



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni