Jumatano, 12 Machi 2014

NGUVU ZAIDI ZAONGEZWA KUITAFUTA NDEGE YA MALAYSIA ILIYOPOTEA TOKA IJUMAA ILIYOPITA

 Zoezi la kuitafuta ndege ya shirika la ndege la Malaysia imeendelea usiku na mchana baharini kwa kushirikisha vikosi vya uokoaji na majeshi ya majini kutoka nchi mbalimbali Ulaya kuitafuta ndege hiyo iliyopoteza mawasiliano masaa mawili tu baada ya kuruka kutoka Kuala Lumpa Malaysia kuelekea Beijing China toka siku ya ijumaa iliyopita.
 Meli kubwa zenye zana zote za uokoaji zimekuwa zikitumika kuitafuta ndege hiyo iliyokuwa na abiria 239 kutoka zaidi ya mataifa 14, huku China ikiwa imepekea mitambo 10 ya satelaiti kwa ajili ya kusaidia kuitafuta ndege hiyo
 Ndege na helkopta za kijeshi pia zimekuwa zikitumika katika zoezi hilo. Mpaka sasa bado kuna giza kubwa mbele kuelewa ukweli wa kupotea kwa ndege hiyo, huku kukiwa na taarifa za kujichanganya, moja zikisema uhenda imetekwa nyara na nyingine zikisema imeanguka baharini

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni