
Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limetangaza kuwa hakutakuwa na suala la kutolewa hotuba katika sherehe za ufunguzi wa Kombe la Dunia mwezi Juni mwaka huu.
Mwaka jana Rais wa Brazil Dilma Rousseff alizomewa na mashabiki wa mpira katika ufunguzi wa Kombe la Shirikisho, ambalo huanza kabla ya michuano ya Kombe la Dunia.
Katika mahojiano na Shirika la Habari la DPA, Rais wa Fifa Sepp Blatter ameonyesha kusikitishwa na hali ya kukosekana kwa utulivu nchini Brazil, hata hivyo anatarajia michuano ya Kombe la Dunia itatuliza hali hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni