Wajumbe wa Bunge maalum la katiba jioni hii wamemchagua Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta kuwa Mwenyekiti wa kudumu wa Bunge maalum la Katiba ambalo linaendelea mjini Dodoma.
Sitta ameshinda nafasi hiyo baada ya kupata kura 487 akimshinda mpinzani wake Hashim Rungwe aliyepata kura 69 sawa na asilimia 12.3 huku kura 7 zikiharibika.
Wajumbe waliopiga kura walikuwa 563 kati ya wajumbe 629
Akiongea baada ya kutangazwa mshindi,Samuel Sitta aliwashukuru wajumbe wote waliompigia kura na kushinda pamoja na Chama Cha Mapinduzi CCM kwa kumpitisha kugombea nafasi hiyo.
Pia alimshukuru Endrew Chenge huku akisema hakukuwa na ushindani mkali kati yao katika kuwania nafasi hiyo ndani ya chama kama ilivyokuwa inavumishwa na watu


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni