Pichani Kati ni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi,Mh.Jaji Mstaafu Damian Lubuva akizungumza mbele ya Waandishi wa habari
mapema leo mchana,kwenye moja ya ukumbi wa mikutano ya Hill Top Hotel,mjini
Iringa kuhusiana na ufafanuzi wa Daftari la Kududumu la Wapiga Kura
litakalotumika katika Uchaguzi wa Ubunge jimbo la Kalenga,unaotarajiwa
kufanyika machi 16 mwaka huu.Jaji Lubuva amebainisha kuwa Tume haijafanya
Uboreshaji kwa maana ya kuandikisha Wapiga kura wapya ambao hawakuwa
wamejiandikisha kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010.
"Kilichofanyika Mwaka 2014 ni Uhakiki wa Daftari hilo
ili kuwa sahihi zaidi na kuhakikisha kila aliyeandikishwa hapo awali na kupewa
kadi ya kupigia kura anatumia haki yake ya kupiga kura,hii ni kuondoa
malalamiko ya kushindwa kupiga kura kwa sababu ya kukosekana jina lake kwenye
Daftari",amesema Jaji Lubuva.Pichani kulia ni Mkurugenzi wa Tume ya Taifa
ya Uchaguzi,Mh.Julius Mallaba na kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa
ya Uchaguzi,Jaji Mstaafu Hamid Mahmoud Hamid.
Amesema kuwa kutokana na Uhakiki uliofanyika,ukweli ni
kwamba taarifa za wapiga kura zilizohakikiwa zilikuwa 149 tu.Wapiga kura
walioongezeka katika Daftari lililotumika katika uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010 ni
saba (7) tu na sio 600 kama ilivyotolewa taarifa kwenye vyombo mbalimbali vya
habari
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni