Jumapili, 9 Machi 2014

UKARIBU WA RIHANNA NA RAPA DRAKE WAZUSHA MINONG'ONO

                             Rihanna akitoka kwenye hoteli aliyokuwa na Drake.
Baada ya kupanda jukwaani pamoja Jijini Paris Rihanna na rapa Drake waliibua minongono kuwa huenda wawili hao wapo kwenye mahusiano, hata kabla ya hilo halijathibitishwa mastaa hao wamezidisha uvumi baada kunaswa wakitoka kula pamoja mlo wa usiku huko Amsterdam.

Wawili hao walinaswa wakitoa kwenye hoteli moja ya Sushi, baada ya kula mlo huo pamoja katika Jiji hilo kuu la nchi ya Uholanzi, ikiwa ni siku moja baada ya Drake kufanya shoo Ziggo Dome kwenye ziara yake ya sasa.
                         Drake akifuatia kwa nyuma baada ya Rihanna kutoka.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni