Watu wanane wamekufa huku wengine wengi
wakijeruhiwa baada ya magari waliyokuwa wakisafiria kugongwa na Lori
kwenye barabara Kuu ya Nakuru-Eldoret alfajiri ya leo.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Polisi wa Kituo
cha Rongai Joseph Mwamburi magari hayo ambayo ni basi la Matatu aina
ya Nissan, Toyota Probox na Lori yalikuwa yakielekea Nakuru ambapo
breki za Lori zilishindwa kufanya kazi na kuyagonga magari hayo
mawili.
Abiria saba waliokuwamo kwenye basi la
Matatu pamoja na mmoja aliyekuwemo kwenye Lori walikufa papo hapo
huku majeruhi wengine wengi wakikimbizwa kwenye hospitali ya Nakuru.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni