Nyota wa Miami Heat LeBron James
maarufu kama King James ametoa kali pale aliposema kutocheza kwake
vizuri katika mchezo wa kikapu waliopoteza dhidi ya San Antonio Spurs
kulichangiwa na jezi mpya za mikono mifupi zilizopendekezwa kwenye
Ligi ya NBA.
James alifanikiwa kutumbukiza mpira
mara sita kati ya 18 aliyojaribu kutikisa nyavu za kikapu wakati Heat
ifungwa111-87. Baada ya mchezo huo James alinukuliwa akisema sitafuti
sababu lakini mimi si mpenzi wa jezi hizi mpya.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni