Alhamisi, 13 Machi 2014

WAKILI WA OSCAR PISTORIUS AHOJI UWEZO WA KITAALUMA WA MCHUNGUZI WA UHALIFU


Wakili wa Oscar Pistorius anayemtetea kwa kosa la kuua katika Mahakama ya Kuu ya Gauteng Kaskazini hii leo ameanza kwa kuhoji uwezo wa kitaaluma wa mchunguzi wa matukio ya uhalifu aliyetoa ushahidi wake jana.

Akijibu swali la Wakili Barry Roux ( picha juu ) anayemtetea Pistorius, Kanali Johannes Vermeulen amesema amehitimu kozi za uchunguzi wa matukio mbalimbali yakiwemo moto, alama na kuoanisha vitu vilivyonyambulika. Pia alihitimu kozi ya kuchunguza ushahidi ya FBI Marekani mwaka 1998.
Vermeulen jana alitoa ushahidi namna ambavyo Pistorius alivyotumia gongo la kuchezea mchezo wa Kriketi kuvunja mlango wa choo baada ya kumpiga risasi mpenzi wake Reeva Steenkamp kwa kudhani kuwa kavamiwa na mtu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni