Alhamisi, 13 Machi 2014

WAUMINI INDIA WAUGANDISHA KWA BARAFU MWILI WA KIONGOZI WAO WAKIAMINI ATAFUFUKA

Waumini watiifu wa mmoja wa Kiongozi wa Kiroho (Guru) nchini India wameugandisha kwa barafu mwili wake baada ya kufa wakiamini kuwa atafufuka na kuendelea kuwaongoza waumini wake.

Guru Ashutosh Maharaj alithibitishwa na Mamlaka ya Punjab kuwa amekufa Januari 29 baada ya kupatwa na shambulio ya moyo, hata hivyo waumini wa dhehebu lake la Divya Jyoti Jagrati Sansthan wapatao milioni 30 wanaamini yupo katika hali ya kuwasiliana na mungu kwa karibu mno.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni