Mahakama nchini Ujerumani imemhukumu
Rais wa Klabu Bingwa Barani Ulaya ya Bayern Munich kifungo cha jela
miaka mitatu na miezi sita kwa kukwepa kodi.
Rais huyo Uli Hoeness alikiri kufanya
udanganyifu wa kodi kwa mamlaka ya kodi ya Ujerumani na
kujilimbikizia mamilioni ya euro.
Hoeness ambaye alikuwemo kwenye kikosi
cha Ujerumani kilichotwaa kombe la dunia, alificha fedha hizo kwa siri kwenye
akaunti ya benki moja ya nchini Swiss.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni