Waziri wa Elimu nchini Kenya Jacob
Kaimenyi amesema hatojiuzulu kama inavyoshinikizwa na wabunge kutokana
na kuhusika na tenda ya ununuzi wa laptop kwa wanafunzi wa shule
yenye mgogoro.
Akiongea na vyombo vya habari leo
Jijini Nairobi Kaimenyi amesema hakuwa na shaka yoyote kuhusiana na
tenda hiyo iliyopewa kampuni ya India ambayo imebainika haina uwezo
wa fedha.
Kampuni hiyo ya India ya Olive
Telecommunications, ilipatiwa kimakosa tenda ya laptop yenye thamani
ya shilingi bilioni 26.4 za Kenya.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni