Kocha Mkuu ya timu ya Yanga, Hans Van
Pluijm ametangaza kikosi kitakachowavaa Al Ahly hii leo huko
Alexandria nchini Misri, bila ya kuwa na kiungo wao machachari Haruna
Niyonzima.
Kwa mujivu wa taarifa kutoka kwenye
kambi ya timu hiyo huko Misri Niyonzima atashindwa kushuka dimbani
kuwavaa waarabu hao kutokana na kuugua ugonjwa wa malaria.
Katika mchezo wa awali uliochezwa
Jijini Dar es Salaam timu ya Yanga iliibuka kidedea kwa kuifunga Al
Ahly bao 1-0 na hii leo inakabiliwa na kibarua kigumu ya kuitoa timu
hiyo katika Ligi ya Klabu Bingwa Afrika na kutinga hatua ya 16 Bora.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni