Watumishi wa umma nchini Kenya wameapa
kupinga uamuzi wa kupunguzwa kiwango cha mishahara yao ili kudhibiti
mzigo mkubwa wa mishahara unaoielemea serikali, licha ya Rais Uhuru
Kenyatta na Naibu wake William Ruto kuagiza nao mishahara yao
ipunguzwe.
Rais Uhuru na Naibu wake Ruto
waliafikiana kukubali kukatwa asilimia 20 ya mshahara yao, ambapo pia
mawaziri wa serikali ya Kenya nao walikubali kupunguzwa asilimia 10
ya mshahara wao katika kudhibiti mzigo wa mishahara ya umma unaozidi
kuongezeka.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni