Mke wa Rais wa Kenya Mama Margaret
Kenyatta leo asubuhi amekimbia katika uzinduzi wa mbio za Marathoni
za Mke wa Rais, zenye lengo la kuboresha huduma za afya kwa
wakinamama wajawazito nchini Kenya.
Mbio hizo zilizofanyika Jijini Nairobi
ni sehemu ya kampeni yake ya “Beyond Zero” iliyoianzisha kwa
ajili ya kununulia kliniki zenye kutembea ili ziweze kutoa huduma
bora za kujifungua na kabla ya kujifungua kwa wajawazito nchini
Kenya.
Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, katika
Kenya wanawake 360 hufa wakati wa kujifungua kati ya wanawake
100,000.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni