Alhamisi, 28 Mei 2015

JESHI LA MAREKANI LAPELEKA KIMAKOSA SAMPULI ZA VIMETA HAI KATIKA MAABARA

Jeshi la Marekani limepeleka kimakosa sampuli za vimeta hai katika maabara tisa katika nchi hiyo na katika kambi ya Marekani nchini Korea Kusini.

Pentagon imesema wanajeshi 22, katika kambi ya anga ya Osan Korea Kusini wanapatiwa tiba ya kinga kutokana na uwezekano wa kupata maambukizi baada ya kukaa na sampuli hizo.

Nchini Marekani raia wanne wanapatiwa matibabu, ingawa inasemekana hawapo katika hatari kubwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni