Rais Robert Mugabe
wa Zimbabwe ameeleza kuwa ni aibu kwa viongozi wa bara la Afrika
kushindwa kumuenzi Baba wa Taifa la Tanzania Mwalimu Julius Nyerere
kwa kujitolea kwake katika kukomboa bara la Afrika.
Rais Mugabe ametoa
kauli hiyo jana katika hafla ya kutimiza miaka 90 ya kuzaliwa kwake
iliyoandaliwa na Ikulu mara baada ya kurejea kutoka Singapore
alipoenda kufanyiwa upasuaji wa jicho lake.
Rais Mugabe
amewataka viongozi wa bara la Afrika kuongeza jitihada zaidi za
kumuenzi Mwalimu Nyerere ambaye aliigeuza nchi yake kuwa kitovu cha
harakati za ukombozi wa nchi za bara la Afrika.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni