
Nchi ya Afrika Kusini imewatuhumu maafisa Ubalozi watatu wa Rwanda iliyowafukuza kwa kuhusika na mauaji pamoja na majaribio ya kuu raia wa Rwanda wanaoishi nchini Afrika Kusini.
Waziri wa Sheria wa Afrika Kusini Jeff Radebe amesema nchi yake inaoushahidi unaowahusisha maafisa hao wa Rwanda na shughuli zilizo kinyume na sheria za nchi.
Maafisa hao wa Ubalozi wa Rwanda nchini Afrika Kusini walifukuzwa Ijumaa kufuatia tukio la shambulio la nyumba ya mkimbizi wa Rwanda, Kayumba Nyamwasa Jijini Johannesburg.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni