
Cristiano Ronaldo ameonyesha usamaria wema kwa kujitolea kulipia gharama za upasuaji za mtoto wa miezi 10, ambaye alikuwa na matatizo ya mfumo wa nyuroni, na wazazi wake walikuwa hawana uwezo.
Mtoto huyo Erik Ortiz Cruz ilikuwa hamna namna ya kuweza kupona bali ni kufanyiwa upasuaji, ambapo vipimo tu viligharimu paundi 5,020 ambapo pamoja na upasuaji gharama zake zinafikia paundi 50,240 sawa na zaidi ya shilingi milioni 13 za Tanzania.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni