Usiku wa kuamkia leo umekuwa mbaya kwa Manchester City baada ya kushuhudia wakifungwa tena mabao 2-1 ugenini katika uwanja wa Camp Nou na Fc Barcelona, matokeo ambayo yameiondoa timu hiyo katika ligi ya mabingwa barani Ulaya huku Barcelona wakisonga mbele hatua ya robo fainali.
Fc Barcelona wamefanikiwa kutinga robo fainali kwa jumla ya mabao 4-1, kwani katika mchezo wa kwanza waliifunga Manchester City mabao 2-0 nyumbani kwao. Mabao ya Barcelona yalifungwa na Lionel Messi dakika ya 67 na Dani Alves 90 huku bao la kufutia machozi la Manchester City likifungwa na Kompany kunako dakika 89
Katika mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi Stephane Lannoy, ulishuhudia mchezaji wa Man City Pabblo Zabaleta akizawadiwa kadi nyekundu dakika ya 78 na kutolewa nje ya uwanja kwa mchezo mbaya
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni