MEGATRADE YAVIPIGA JEKI VILABU VYA POLISI KILIMANJARO NA MACHAVA FC VYA MJINI MOSHI
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama akimkabidhi jezi nahodha wa timu ya Machava ,Dickson Muganda.Jezi hizo zenye thamani ya kiasi cha sh Milioni 3 zimetolewa na kampuni ya Megatrade ikiwa ni sehemu ya msaada kwa timu hiyo inayoshiriki ligi daraja la tatu ngazi ya mkoa wa Kilimanjaro.
Meneja masoko wa kampuni ya Megatrade (T) Ltd,Goodluck Kway akikabidhi hundi ya sh Milioni 3 kwa kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz ikiwa ni sehemu ya msaada kwa timu ya soka ya Polisi Kilimanjaro inayoshiriki ligi daraja la tatu ngazi ya mkoa wa Kilimanjaro.shoto kwake ni Meneja mauzo wa Kampuni ya Megatrade(T)Ltd kanda ya kaskazini Edimund Lutaraka
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni