Ujumbe kutoka Umoja wa Ulaya kupitia European Investment
Bank (EIB) wiki hii umetembelea Wizara ya Maji na kukutana na Waziri wa Maji,
Prof. Jumanne Maghembe ofisini kwake.
Ujumbe huu uliongozwa na Makamu Rais wa EIB, Pim van
Ballekom kutoka Luxembourg akifuatana na wawakilishi wengine Richard Willis,
Catherine Colllin, Cristian Mejia-Garcia na Anne Claire Dauvier, Adam
Grodzicki.
EIB inatoa msaada kwa
miradi ya Sekta ya Maji nchini katika kufanikisha utekelezaji wa miradi hiyo
ambayo inaendelea hapa nchini ikiwemo katika miji ya Mwanza, Bukoba na Musoma.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni