Msako mkali umeendelea baharini kati ya Malaysia na Vietnam kutafuta ndege ya shirika la ndege la Malaysia Airline iliyopotoea toka imeondoka mjini Kuala Lumpar kuelekea Beijing nchini China. Ndege hiyo Boeng 777 ilikuwa na abiria 239, na ilipoteza mawasiliano masaa mawili baada ya kuruka
Uchunguzi mkali umekuwa ukifanyika baharini kuangalia kama ndege hiyo ilianguka, na taarifa zinasema kuwa maofisa wa Vietnam wamesema wameona michirizi mikubwa ya mafuta katika bahari nje ya mwambao kusini mwa nchi hiyo, taarifa ambayo inaweza kutafsiriwa kuwa ndege hiyo ilianguka baharini, japo bado taarifa hizo hazijathibitishwa na upande wowote
Marekani nayo imejitokeza kusaidia uchunguzi wa kuitafuta ndege hiyo baada ya kutoa meli yake ya kijeshi ili isaidie katika uchunguzi huo kama inavyoonekana pichani juu. Rweyunga Blog tunaendelea kuifuatilia taarifa hii kwa ukaribu na tutawajulisha wasomaji wetu
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni