.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 12 Machi 2014

NMB YAWAKOMBOA VIJANA KIUCHUMI KWA KUWAPA MIKOPO NAFUU YA PIKIPIKI


Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu uwekezaji na uwezeshwaji, Mhe. Dkt Mary Nagu akikata utepe kama ishara ya ufunguzi rasmi wa uwezeshwaji kwa wateja wa NMB kupitia mikopo ya pikipiki za miguu miwili na mitatu kutoka benki ya NMB. Uzinduzi huo ulifanyika katika hoteli ya Tilapia ya jijini Mwanza

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mikopo hii jijini Mwanza, Waziri wa Uwezeshaji na Uwekezaji kutoka ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Dkt. Mary Nagu amesema “Mikopo hii ya pikipiki itawasaidia sana vijana na wananchi kwa ujumla kuweza kumiliki pikipiki zitakazowawezesha kuendesha maisha yao ya kila siku. Binafsi natambua ajira kwa vijana imekua ni changamoto maeneo mengi nchini hivyo basi ningependa kuwasisitiza vijana wachukue fursa hii inayotolewa na NMB kuweza kumiliki biashara zao wenyewe na kujikimu kiuchumi.”
Mkuu wa Kitengo cha Biashara za benki ya NMB, Bw. Filbert Mponzi wakati wa uzinduzi wa mpango wa uwezeshwaji kwa wateja wa NMB kupitia mikopo ya pikipiki za miguu miwili na mitatu kutoka benki ya NMB. Kushoto ni Meneja wa NMB Kanda ya ziwa, Bw. Straton Chilongola.

Marejesho ya mkopo huu wa pikipiki ya miguu miwili na mitatu yanatolewa ndani ya muda wa miezi 24, ambapo kwa kipindi hiki chote, mteja ataendelea kurejesha makato yake ya kila mwezi kwakuzingatia taratibu za makubaliano yatakayofanyika baina ya mteja na benki ya NMB.
Mikopo hii pia inawekewa bima kwa ajili ya ulemavu au kifo kitakachomtokea mmliki wa pikipiki iliyochukuliwa mkopo. Bima hii ni kwaajili ya kumpa unafuu mkopaji endapo atapata matatizo ya kiafya ambayo yatamfanya apate ulemavu au kupoteza maisha.

Mikopo hii yenye masharti nafuu inatolewa kwa mteja yeyote ambaye atatitimiza vigezo vilivyowekwa ili kupata mkopo huu. Anachotakiwa kufanya mteja ni kulipia asilimia thelathini ( 30%) ya bei ya pikipiki ya miguu miwili au mitatu kama inavyouzwa na wasambazaji wa pikipiki hizi za Fair Deal Auto Private Ltd , Car & General Ltd pamoja na Quality Motors.

Kwa maelezo zaidi temmbelea matawi ishirini na moja tu ya NMB nchi nzima yanayotoa mikopo hii kama ifuatavyo: Mwanza-Buzuruga na Kenyata Road,

Dar es Salaam-Tegeta, Magomeni, Mwenge, Mbezi Beach, Temeke, Ilala, Mlimani City, Msasani na Airport

Arusha-Clock Tower na Arusha Market

Manyara-Babati na Katesh

Dodoma

Mbeya-Mwanjelwa, Mbalizi Road na Usongwe

Moshi-Nelson Mandela na Tanga-Madaraka

NMB BENKI YAKO

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni