Ndani ya ukumbi wa Bunge maalum la Katiba zoezi linalofanyika hivi sasa ni kupiga kura kwa wagombea waliojitokeza kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa kudumu ambaye ataliongoza Bunge hilo.
Wagombea waliojitokeza kuwania nafasi hiyo ni Samweli Sitta na Hashim Rungwe na wote wamejitokeza mbele na kujieleza kwa ufasaha mkubwa pamoja na kujibu maswali waliyoulizwa na wajumbe wa bunge hilo maalum la katiba.
Wa kwanza kujieleza alikuwa Hashim Rungwe na kufuatiwa na Samweli Sitta ambaye alionekana kuwateka zaidi wajumbe kwa maelezo yake huku akijinadi yeye ni mtu wa viwango na anajulikana kwa hilo.
Tutawapa matokeo pindi yatakapotoka, fuatilia hapa hapa Rweyunga Blog.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni