
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry anajiandaa kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov Jijini London, wakati mgogoro wa kura ya maoni ya jimbo la Crimea kujitenga ukishika kasi.
Kerry anatarajiwa kumuonya Lavrov kuwa kura hiyo ya maoni na kitendo cha Urusi kuingiza jeshi Crimea na itapelekea kuwepo kwa vikwazo vya Marekani na Umoja wa Ulaya.
Kerry ameonya hatua kali iwapo Urusi italigawa jimbo la Crimea, ambalo linatarajia kupiga kura ya maoni ya kujitenga na Ukraine ili kujiunga na Urusi baadaye mwezi huu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni