Maofisa wa Benki ya CRDB wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Dk. Charles Kimei wakiwa katika ibada maalumu ya kuchangisha fedha kwa ajili ya Kanisa la KKKT jimbo la Hai.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti,Huduma kwa Wateja Tully Mwambapa akiwasili katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Jimbo la Hai kwa ajili ya ibada maalumu ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa la KKKT jimbo la Hai. Katika harambee hiyo Benki ya CRDB ilitoa shilingi milioni 20 kufanikisha ujenzi wa Kanisa na Kituo cha Watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Kanisa la KKKT jimbo la Hai.
Baadhi ya waumini wakiingia kanisani wakati wa ibada maalumu ya iliyofanyika katika Kanisa la KKKT jimbo la Hai, iliyokwenda sambasamba na harambee ya kuchangia kanisa hilo pamoja na Kituo cha Watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni