Jaji wa Afrika Kusini anayesikiliza
kesi ya Oscar Pistorius amemuagiza kuanza kufanyiwa vipomo kila siku
kuanzia jumatatu, ili kubaini hali ya akili yake wakati alipomuua
mpenzi wake mwaka jana.
Jaji Thokozile Masipa amemuamnia
mwanariadha huyo anayetumia miguu ya bandia, kwenda Hospitali ya
wagonjwa wa akili ya Weskoppies iliyopo Pretoria kama mgonjwa wa nje
kwa muda wa mwezi mmoja.
Uamuzi huo wa Jaji Masipa umekuja
baada ya upande wa utetezi kudai Pistorius anasumbuliwa na tatizo la
kujawa na hofu. Katika kesi hiyo Pistorius amekanusha shtaka la
kumuua kwa makusudi mpenzi wake Reeva Steenkamp.
Reeva akiwa na Pistorius wakati wa uhai wake
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni