.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 21 Mei 2014

KINANA AZINDUA NYUMBA YA KISASA YA MFUGAJI ALIYEZINDUKA KWA SERA ZA CCM HUKO MANYONI

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo, Mei 20, 2014, kwenye Viwanja vya Stendi mjini Manyoni, akiwa katika siku yake ya pili ya ziara ya siku nane mkoani Singida, kwa lengo la kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi huku akijadiliana nao njia ya kuzitatua mkoani humo.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia kwenye mkutano huo leo.
Kinana akipewa zawadi ya zana za asili na mzee mmoja wa Kijiji cha Heka, wilayani Mnyoni leo.
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akimpa tofali fundi aliposhiriki ujenzi wa maabara ya shule ya Sekondari Heka, Manyoni, Mei 20, 2014 wakati wa ziara hiyo.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida, Mgana Msindai (kushoto) akimpatoa tofali Nape ili kumpatia fundi wakati wa kushiriki kwenye ujenzi wa chumba cha maabara ya shule hiyo ya Heka.

Nape akimpatia fundi tofali kwenye kushiriki ujenzi wa chumba hicho cha maabara katika shule hiyo ya Heka, leo Mei 20, 2014.
Kinana akizindua nyumba ya mpya ya kisasa ya mfugaji Jonase Mihangwa wa Kijiji cha Heka, wilayani Manyoni ambye  ambaye amekuwa miongoni mwa wafugaji wa kuigwa kwa kuamua kuuza sehemu ya mifugo yake kubadilisha maisha yake ikiwemokujenga nyumba hiyo ya kisasa yenye umeme wa mionzi ya  jua.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni